figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Kwa ufupi
- Kiwango cha juu alichokionyesha Mbaraka kimewavutia Simba, Yanga na Singida United kila moja ilionyesha nia ya kutaka kumsajili.
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, imemalizana na mshambuliaji Mbaraka Yusuph kwa mkataba wa miaka miwili.
Mbaraka aliyefunga mabao 12 msimu uliopita wa Ligi Kuu amemaliza mkataba wake Kagera Sugar.
Kiwango cha juu alichokionyesha Mbaraka kimewavutia Simba, Yanga na Singida United kila moja ilionyesha nia ya kutaka kumsajili.
Katika harakati hizo Yanga ilitangaza kumpa Sh 50 milioni, Singida United ingetoa Sh 40 milioni wakati ofa ya Simba haikuwekwa wazi.
Matatizo ya kiuchumi inayopitia Yanga kwa sasa imewafanya mabingwa hao kujiondoa katika mbio za kumnasa mshambuliaji huyo.
Habari za uhakika zinasema Azam baada ya kuipata saini ya Mbaraka watamtambulisho kesho Jumapili.
Uamuzi wa kumtambulisha kesho unatokana na mshambuliaji huyo kuwa katika majukumu ya timu ya Taifa 'Taifa Stars' itakayocheza kesho, Jumamosi dhidi ya Lesotho ikiwa ni mechi ya kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia 2019.
Chanzo: Mwananchi