Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kile kipande cha agizo la Rais John Magufuli kwa TANESCO kuhusu ukataji umeme, kinachorushwa kabla ya taarifa za habari za saa mbili usiku za runinga zetu, kinao ujumbe mkubwa sana unaohitaji jicho la tatu kuweza kuubaini.
Mheshimiwa Rais anasikika akiwaambia TANESCO wafanye kazi kwa mujibu wa "professions" zao. Waheshimu taaluma zao kwanza kabla ya kutanguliza urafiki na undugu. Hapo kwenye kutanguliza taaluma kwanza, ni sehemu ambayo kwa kweli ni ugonjwa wetu wa muda mrefu.
Vifo vya mashirika ya umma katika awamu zilizotangulia, chanzo chake ni taaluma za watu kuingiliwa na aidha wanasiasa au marafiki zao. Na watu hao bado wapo, kibaya zaidi ni maadui wa mfumo wa kimaisha wenye kuzingatia tija yenye faida kwa wananchi wengi, kwa kupitia mizania ya haki.
Jambo lingine bora zaidi ni kwamba pamoja na udhaifu wa awamu ya tano kwenye baadhi ya maamuzi, ipo ile heshima ya taaluma ya mtu. Na mwenye elimu pana ya kitu fulani anao uhuru wa kufanya kazi itakayoacha kumbukizi itakayodumu kwa miongo mingi ijayo.
Naamini kwamba hii dhana ya awamu ya tano ya kuwa tayari kuipatia taaluma ule uhuru wa kuzaa matunda, itakuja kuwa na matokeo chanya na ya moja kwa moja kwenye maisha ya watanzania wengi. Ni suala la kuiamini dhana hii.
Wenzetu Kenya kwa mfano, wanaweza kuwa na siasa zao za makundi na za kikabila lakini kamwe hawakubali kuyashusha thamani mambo yote yenye uhusiano wa moja kwa moja na taaluma za watu. Kwenye utalii wataweka mbobezi wa utalii, kwenye anga wataweka mbobezi wa anga, kwenye afya atawekwa mjuzi wa afya.
Tulizoea maisha ya kuingilia ufanisi wa utendaji kazi wa watu, tukidhani kuwa mambo ya kitaaluma yanaweza kufanyika kienyeji tu, matokeo yake tumechelewa kuanza kuzikimbia zile mbio za kutafuta maendeleo halisi.
Tusije kurogwa kwa namna yoyote ile tukadhani kuwa mazoea yetu ya miaka ya nyuma yalikuwa ni sahihi. Tutarudi kule kule kwenye vurugu mechi za kila sekta.
Nawatakia Pasaka njema yenye mapumziko ya nyumbani yasiyo na lolote lile ambalo ni baya.