JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
salamus !
Binafsi napenda kutoa pongezi za dhati kwa namna Serikali ya awamu ya tano ilivyo anza kufanyakazi zake kwa kujituma na kusimamia uwajibikaji serikalini.Hongera sana mheshimiwa Rais JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.
Napenda nitoe ushauri ufuatao. Ningependa sana awamu ya tano iwe ni awamu ya kusimamia uchumi,uwajibikaji na nidhamu serikalini.serikali iliyo simamiwa vizuri huleta matokeo mazuri kiuchumi, kijamii na kisiasa.Katika uwajibikaji ubunifu liwe ni jambo linalo pewa kipaumbele!Nitatolea mfano.
Iwe ni aibu kukuta shule ina choo kinacho tumiwa kwa pamoja walimu na wanafunzi wakati shule hiyo ina mkuu wa shule na bodi ya shule ipo! hiyo ikitokea ujue kwamba watu hawa wamekalia talanta na kamwe hawawezi kuleta maendeleo, wanastahili kufukuzwa kazi wote.Bank zipo kwanini mkuu wa shule na bodi yake wasikae chini waka chukua mkopo Bank ,wakakubaliana kulipa deni polepole mpaka deni litakapo isha na shule ikawa imepata vyoo kwajili ya wanafunzi na wafanyakazi peke yao? iwe ni aibu kukuta jengo la serikali limechakaa kwa kushindwa tu kupaka rangi.Angalia majengo ya TRL, POLISI NA NYUMBA ZA WALIMU.
UCHUMI ni lazima usimamiwe. Halmashauri ziwekewe majukumu katika kupanga, kusimamia na kukuza uchumi wa watu katika maeneo yao.Iwe ni aibu kwa Halmashauri kutegemea kimapato serikali kuu kwa asilimia 50.Iwe ni aibu kwa Halmashauri iliyo zungukwa na bahari au maziwa makubwa lakini hakuna vikundi vya watu wanao vua samaki kwa kiwango cha biashara(Large scale fishing).wahamasishe ukuaji wa uchumi ili baadae wapate vyanzo imara na endelevu vya kodi.Halimashauri ziwekewe malengo na mkurugenzi asiye weza kutimiza malengo aondolewe kazini.
uwajibikaji serikalini bado uko chini sana hasahasa miongoni mwa watumishi wa umma.Kuna watu hawatimizi majukumu yao ipasavyo.Nitatolea mfano,Fedha za Tanzania zimechakaa sana hasa noti za shs 500,1000, 2000 na kwa kiwango kidogo nti za shs5000.Lakini Bank kuu wapo tu hawajawahi kuwafundisha watanzania hasa waishio vijijini namna bora ya kutunza fedha za karatasi yaani notes! Fedha zisipo tunzwa huchakaa mapema na kuchapa noti mpya ni ghali na husababisha thamani ya fedha yetu kushuka.WAAMKE WAWAJIBIKE, WATOE ELIMU KWA UMMA JINSI YA KUTUMIA WALLETS KUHIFADHI FEDHA ILI ZIDUMU,Lakini pia wahimize matumizi ya electronic transactions maeneo ya mjini kwa bidhaa karibu zote, inawezekana.
Nina matumaini makubwa na serikali yako Mheshiwa Rais na bila shaka muda siyo mrefu Jiji la Dar litapendeza kwasababu ya hatua mujaarabu unazo chukua sasa.Himiza ubunifu miongoni mwa watumishi wa Halmashauri zote,Mpango wa kusimamia ukusanyaji mapato utakufanya ujenge serikali yenye heshima duniani.