Awamu ya 5 na "Michakato!"

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,976
Awamu hii niliamini kuwa haina mambo ya "Michakato" kama Raia Na 1 alivyotuaminisha hasa wakati wa Kampeni ya kuingia Nyumba nyeupe! Alisikika akisema kuwa atakayeendekeza "michakato" "atatimuliwa kazi ili akafanyie michakato huko huko!"
Kumbe ahadi na uhalisia ni vitu tofauti!

1. Sasa hivi kupandishwa vyeo kumesimamishwa ili "mchakato" wa uhakiki wa watumishi hewa ukamilike!

2. Ajira mpya zimesimamishwa ili kupisha "mchakato" wa uhakiki wa watumishi hewa ukamilike!

3. Kupandishiwa mishahara kumesimamishwa ili kupisha "mchakato" wa uhakiki...ukamilike!

4. Sasa hivi watumishi wa Serikali wanasimamishwa kazi ili kupisha "uchunguzi" (mchakato)...

5.........
Hongereni wahusika kwa "michakato" murua ila 2020 msije kudai kuwa hakuna tena "michakato!"
 
Usistaajabu ya Mussa utawaona ya firauni polepole utaanza mchakato wa kuondoa chuki na visasi miongoni mwa wanasiasa, kutanabahi miaka mitano kushneh!!!
 
Tangu tupate uhuru, sijaona awamu ya HOVYO kama hii ya baba Jesca. Yaani hakuna la maana zaidi ya kupenda sifa za kijinga. Kila wanalofanya wanakosea.
 
Na kuhusu janga lililowapata watu Kagera - Bukoba,

Yuko wapi huyu Rais? Hajajitokeza kusema lolote kabisa!!

Sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi ni manispaa ya Bukoba ambayo wakazi wake walimnyima kura wakawapa CHADEMA..

Hivi inawezekana akawa na "allergy" na maeneo yanayoongozwa na CHADEMA kwa kiwango hiki hata asitambue kuwa yeye ni "Rais wa wote" bila kujali itikadi zao sawasawa na kiapo chake??

Ukimya wa "Mtukufu" Rais ktk hili unatia shaka sana.

Labda kama anaumwa, basi hiyo ni kesi nyingine Mungu anisamehe maana kuugua nako ni "natural hazard" sawasawa na tetemeko la ardhi!!

Lakini kama ni mzima tu, reaction yake ktk hili inatia shaka saaaaana!!
 


Kuna watu bado tuna ikumbuka ile miaka 1O ya Mkwere...... Si kwa kuwa ilikuwa na Unafuu au Neema fulani! La hasha!
Bali ilikuwa ni miaka yenye uafadhali wa Matatizo ukilinganisha na Kipindi hiki cha Baba.J
 
Kuna wakati hali inakuwa mbaya nyumbani hadi baba anaamua kujificha. Ukata mbaya sana.
 
Usistaajabu ya Mussa utawaona ya firauni polepole utaanza mchakato wa kuondoa chuki na visasi miongoni mwa wanasiasa, kutanabahi miaka mitano kushneh!!!

hapo ndipo watakuja kushituka kuwa hawajafanya lolote la maana kwa wananchi kwa sababu ya MCHAKATO!!!!
 
Haya nenda kaawimbie kua waliokutuma wamekosea kukuambia useme kwa kuwa wao hawafirii mwanzo na mwisho wa safari wanachokijua ni propaganda tuu basi
 
We mnafiki tuu.....Umepigwa chini huko Lumumba....Sasa hivi na wewe unaisoma number ehh..
 
Wana mambo mengi mno kwa wakti mmoja. wangekuwa scientific wangechukua agenda chache zilizo ndani ya uwezo wa serikali wakazifanyia kazi hdi mwisho ndio baada ya tathimini wangechukua agenda zingine. Nina masaka kama watafanikiwa kwenye jambo lolote.Kwa mfano wanasema wanataka Tanzania ya viwanda, viwanda gani? tunazo malighafi za kutosha za hivyo imaginary viwanda? huwezi kuwa na kiwanda wakati huna mali ghafi za kupeleka huko.
 
We mnafiki tuu.....Umepigwa chini hiko Lumumba....Sasa hivi na wewe unaisoma number ehh..
Ungejua mimi sijawahi kufika ata huko Lumumba ungekaa kimya ila kwakuwa kiwango chako cha kufikiria imeishia hapo haina budi kuendelea kubishana nawewe
 
Muache propaganda hivii nyie tafiti gani mmefanya ya kisayansi iliowasadia kujenga chama chemu na kuweza kuwashawishi watanzania kila siku ni propaganda hatutafikaa kwa hii hali
 
tokaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…