Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
.
Na; Solomon Michael Kambarangwe
20/06/2016
Watanzania tumeingia awamu ya mpya iliyojaa ahadi lukuki zilizowaaminisha Wananchi kuwa CCM itatekereza iliyoahidi na yaliyodhairiwa kufanywa na vyama vya UKAWA.
Uchaguzi ukachakachuliwa tume ikamtangaza mgombea walioamua kumtangaza kuwa achukue urais. UKAWA hatukukubali matokeo.
CCM kwa kauli mbiu ya Hapa Kazi tu wakaanza kutumia nguvu badala ya akili.
Ziara zilizopewa jina la kushitukiza na mbwembwe kupitia vyombo vya habari na wananchi wakajawa na upepo kuwa sasa ni hapa kazi tu.
Hoja yangu ni kuwa tafsiri ya hapa kazi tu haionekani kabisa. Unapokuwa kiongozi mkuu ukaishia kutishia subordinates wako, kutishia watu, kulazimisha mambo yaende bila mfumo imara wa sheria, sera, kanuni na taratibu rafiki katika miongozo ya uendeshaji wa mamlaka za umma niutapeli wa kisiasa maana huwezi kufanya lolote la maana.
Sasa rais Magufuli analazimisha kufanya mambo kwa utaratibu wa zima moto, akiwa na husuda dhidi ya UKAWA na kuwafanya maadui zake.
Rais Magufuli ameunda serikali na kuwaagiza wateule wake wafanye anayoyataka yeye ambayo mengi ni kinyume cha sheria hasa katika suala zima la madaraka, demokrasia na utawala bora.....hizi ni siasa za kitapeli.
Ukiona bajeti ya serikali imejaa nadharia nyingi. Inayotia kichefuchefu ni ile ya pesa.....imejaa siasa na maneno ya kushawoshi huruma badala ya kuanisha namna ya kujenga uchumi imara.
Serikali iliahidi kutoa elimu bure hadi kidato cha nne ila imeshindwa kugharimia madawati.....sasa tutegemee
*madarasa yatakuwaje?
*nyumba za walimu?
*Maji mashuleni?
*vyoo mashuleni?
*ofisi za walimu?
*samani za ofisi za walimu?
*Mishahara ya walimu?
*Huduma za afya na lishe mashuleni?
Swali ni je wananchi tumeshiriki kuchangia madawati.....tutachangia hayo yote pia?
Huwezi kuboresha elimu kwa kuongeza madawati tu. Jambo kubwa kuliko yote ni mishahara ya walimu, na mazingira yao ya kufanyia kazi.
Ukiiona bajeti ya wizara ya elimu ni ndogo mno kulinganisha na mahitaji halisi ya kuboresha elimu nchini. yaani haina uwezo hata wa kukidhi 30% ya mahitaji ya elimu.
Sasa unaposema unatatekereza dhana ya hapa kazi tu.....kwa utaratibu gani kama sio utapeli wa kisiasa?
Ukienda katika wizara ya afya huko ni majanga tu.. kumejaa matumaini tu na kuhamasisha kujifunga mkanda.
*Wazee, watoto na akina mama wajawazito waliahidiwa kutibiwa bure ila imeishia kwenye majukwaa ya kampeini....siasa za kitapeli.
Mahospitali, zahanati na vituo vya afya tusitegemee jipya kwa mujibu wa bajeti hii. pesa ni ndogo na mbaya zaidi fedha ya Tanzania imeshuka sana thamani.....
Kilimo ndicho binafsi naona kinakwisha kabisa. naona giza tu sekta ambayo ingekwamua uchumi wa wananchi wengi.
Serikali imegawanya fedha kwa utaratibu ambao haunipi matumaini kabisa maana serikali inatumia fedha nyingi kuliko kuziweka katika mafumizi ya maendeleo ya umma.
Nitarudi baadae kumalizia kuandika mada yangu