Avengers: Infinity War itakuwa na sehemu ya pili?

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16,607
Reaction score
27,605
Jana nilienda cinema kuangalia filamu ya Avengers. Jamani hata lile shetani lijambazi sugu halijakufa picha ikaisha. Halafu watu wengine wakaanza kuyeyuka; King of Wakanda akayeyuka kidogo nilie. Wengi waliyeyuka jamani!



Nauliza hivi watatoa part two kweli? Na hilo lishetani limefanikiwa kuchukua vile vidani vyote sita, waliungana wote kulipiga lakini liliwapiga. Pia sehemu niliyofurahia pale kwa Wakanda ule ukuta ni balaa na umoja wao.

Nimeifurahia maana wapo mastar kibao walioigiza Captain America, Thor, Spiderman na wengineo.



Jamani mi movie za kibongo sijui kiafrica zinisamehe kweli. Naomba watoe nyingine nimalizie mimi
 
Sinema yako mama Sabrina na G imefikia wapi[emoji23] [emoji23]
 
Movie tamu kinoma... hapo namkubali sana Doctor Strange..... Ila nimesikitika alivotolewa.

Ile korabo ya Tony Stark, Spiderman, Doctor Strange, Star lord na wenzake ilikuwa imemzidi nguvu Thanos....

Pia Thor kanifurahisha sana na mzuka na miguvu aliyokuja nayo hadi kafanikiwa kumjeruhi Thanos.

Mimi nadhani sehemu ya pili washiriki wote waliotolewa au kufa watarudishwa kwa kutumia ile time stone....

Marvel wako vizuribkwa movies zao na nasubiri kwa hamu mwakani... [emoji51] [emoji51] [emoji51]
 


Yaan hii ilikuwa ngumi mwanzo mwishooo
 
Thanos sio adui ..alikuwa anataka kubalance ulimwengu kwa kupunguza idadi ya viumbe..Nia yake ni nzuri
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…