AUDIO: Mahojiano ya Haji Manara na Kitenge kuhusu utata mechi ya Yanga na Ndanda, mzozo uliopo Simba

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Haya yalikuwa mahojiano tata sana kati ya msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara na mtangazaji wa EFM Maulid Kitenge.

Ni baada ya kumalizika na kwa mechi kati ya Simba na maji maji ambapo timu hizo zilitoka sare.

Kiufupi wamejibizana vikali sana katika ikiwemo suala la mechi ya Yanga na Ndanda kubadili uwanja. Pia suala la mzozo unaoendelea katika klabu ya Simba ambapo Manara anaeleza watazungumza na wanachama punde msimu wa ligi utakapokwisha.

Mwisho wa mahojianoManara anaonekana kuwaka hasira sana hapa.

Naweza kusema ile kauli mbiu ya huu mchezo hauhitaji hasira inajidhihirisha!
 
Attachments

  • Manara na kitenge.m4a
    511.3 KB · Views: 116
Hao ni watani jadi, mmoja anachekelea ubingwa na mwingine ana uchungu ku-moyo ... Tutasikia mengi sasa .. Ngoja tusubiri ..
 
Namuonea huruma sana Haji
Ukiwachilia mbali hasira, Manara anaweza kuwa ana hoja: kwamba VPL imejaa maamuzi ya kushtukiza na/au yenye utata. Anachosahau (au anachojisahaulisha) ni kwamba ghafla na utata huu si kwa Yanga tu. Anajisahaulisha kwamba Azam waliruhusiwa kuacha Ligi ghafla na kwenda kucheza 'Ndondo Cup' Zambia, au kwamba ghafla kanuni ilibadilishwa ili Simba iamue mchezaji wake mwenye tatu za njano akose mechi ipi na baada ya hapo kanuni hiyo ya siri ikafutwa kabisa. Tuwe wakweli, TFF inazibeba sana timu tatu hizi, na kwa hivyo mojawapo yao haipaswi kulia wivu mwenzake anapobebwa. Sanasana ijiandae kununua ubeleko mpya, maana si aghlabu kwa TFF kutumia ubeleko huohuo mara mbili kuzibebea timu hizi!
 
Moja ya kosa wanalolifanya simba ni kusahau mattzo yao na kujari mambo ya yanga au kuwafanya wanachama wao wahisi wanaonewa walilalamika viporo likaisha sasa iv wamekuja na kuhamishwa mechi *
Hii ni sawa na baba kushindwa kutekeleza majukumu ya familia yake ana singizia jiran anamroga
 
Ukiwachilia mbali hasira, Manara anaweza kuwa ana hoja: kwamba VPL imejaa maamuzi ya kushtukiza na/au yenye utata. Anachosahau (au anachojisahaulisha) ni kwamba ghafla na utata huu si kwa Yanga tu. Anajisahaulisha kwamba Azam waliruhusiwa kuacha Ligi ghafla na kwenda kucheza 'Ndondo Cup' Zambia, au kwamba ghafla kanuni ilibadilishwa ili Simba iamue mchezaji wake mwenye tatu za njano akose mechi ipi na baada ya hapo kanuni hiyo ya siri ikafutwa kabisa. Tuwe wakweli, TFF inazibeba sana timu tatu hizi, na kwa hivyo mojawapo yao haipaswi kulia wivu mwenzake anapobebwa. Sanasana ijiandae kununua ubeleko mpya, maana si aghlabu kwa TFF kutumia ubeleko huohuo mara mbili kuzibebea timu hizi!
Well said
 
Jamani simba inahitaji msaada la sivyo itafutika kwenye ramani ya soka!
 
Ukiwachilia mbali hasira, Manara anaweza kuwa ana hoja: kwamba VPL imejaa maamuzi ya kushtukiza na/au yenye utata. Anachosahau (au anachojisahaulisha) ni kwamba ghafla na utata huu si kwa Yanga tu. Anajisahaulisha kwamba Azam waliruhusiwa kuacha Ligi ghafla na kwenda kucheza 'Ndondo Cup' Zambia, au kwamba ghafla kanuni ilibadilishwa ili Simba iamue mchezaji wake mwenye tatu za njano akose mechi ipi na baada ya hapo kanuni hiyo ya siri ikafutwa kabisa. Tuwe wakweli, TFF inazibeba sana timu tatu hizi, na kwa hivyo mojawapo yao haipaswi kulia wivu mwenzake anapobebwa. Sanasana ijiandae kununua ubeleko mpya, maana si aghlabu kwa TFF kutumia ubeleko huohuo mara mbili kuzibebea timu hizi!

Yaani unachotaka kusema wewe Yanga anapobebwa Simba na Azam wakae kimya. Au Simba Anapobebwa Yanga na Azam wake kimya? Hakuna kitu kama hicho kila kitu na wakati wake na kosa moja halihalalishi kosa jingine. Utakuwa ni upuuzi leo hii tuache kujadili hiki kituko cha mwaka cha kubadilishwa uwanja wa kutoka Nangwanda Sijaona kuja Taifa eti kwa sababu mwaka juzi kulikuwa na sheria ya kadi iliyobadilishwa.

Nadhani mada ya sasa ni suala la uwanja wa Ndanda na kuboronga kwa Simba katika ligi hii, hata mambo ya safari ya Azam yalishajadiliwa sana na almost yako closed, labda kwa reference tu.
 
Watangazaji na waandishi hawajiheshimu
na wasemaji wa vilabu nao walewale

Ukiwa msemaji wa Simba na mechi inahusu Simba na Majimaji
hukutakiwa kabisa kuitaja Yanga...
wala mtangazaji hakupaswa kabisa kuileta Yanga hapo

Tuheshimu timu zingine
Majimaji walipaswa kupewa heshima yao ya kutoka na point moja na Simba....
 
SIMBA YA YANGA NI TIMU ZA MPIRA WA MIGUU ZA HOVYO KUWAHI KUTOKEA DUNIANI.
 
Watangazaji na waandishi hawajiheshimu
na wasemaji wa vilabu nao walewale

Ukiwa msemaji wa Simba na mechi inahusu Simba na Majimaji
hukutakiwa kabisa kuitaja Yanga...
wala mtangazaji hakupaswa kabisa kuileta Yanga hapo

Tuheshimu timu zingine
Majimaji walipaswa kupewa heshima yao ya kutoka na point moja na Simba....

Good observation. Manara ameonesha udhaifu mkubwa katika hili. Nadhani huu ni mwendelezo wa vituko kutoka kwa wasemaji wa hizi timu zinazoitwa kongwe kuonyesha kuwa ni "watu wa mpira" zaidi badala ya kuwa weledi. Huwezi kukuta issue kama hizi sio Ulaya tu, bali hata kwa timu za hapa hapa karibu Africa au hata za nchini kama wasemaji wa Azam, Coastal Union, Stand United, n.k
 
TFF walikuwa na nia nzuri but hili limeshaharibika

Huwezi kukuta msemaji wa Man U au Chelsea maarufu kuliko kocha na wachezaji

ni bora tufute hawa wasemaji....
 
Yaani unachotaka kusema wewe Yanga anapobebwa Simba na Azam wakae kimya. Au Simba Anapobebwa Yanga na Azam wake kimya? Hakuna kitu kama hicho kila kitu na wakati wake na kosa moja halihalalishi kosa jingine. Utakuwa ni upuuzi leo hii tuache kujadili hiki kituko cha mwaka cha kubadilishwa uwanja wa kutoka Nangwanda Sijaona kuja Taifa eti kwa sababu mwaka juzi kulikuwa na sheria ya kadi iliyobadilishwa.

Nadhani mada ya sasa ni suala la uwanja wa Ndanda na kuboronga kwa Simba katika ligi hii, hata mambo ya safari ya Azam yalishajadiliwa sana na almost yako closed, labda kwa reference tu.
Hoja yangu ni kwamba wote wasibebwe ili wote wakae kimya. Ila kama wote wanaamua kubebwa basi pia wote wakae kimya. Mwenye haki ya kulalamika ni yule asiyebebwa hata kidogo.
 
Ukiwachilia mbali hasira, Manara anaweza kuwa ana hoja: kwamba VPL imejaa maamuzi ya kushtukiza na/au yenye utata. Anachosahau (au anachojisahaulisha) ni kwamba ghafla na utata huu si kwa Yanga tu. Anajisahaulisha kwamba Azam waliruhusiwa kuacha Ligi ghafla na kwenda kucheza 'Ndondo Cup' Zambia, au kwamba ghafla kanuni ilibadilishwa ili Simba iamue mchezaji wake mwenye tatu za njano akose mechi ipi na baada ya hapo kanuni hiyo ya siri ikafutwa kabisa. Tuwe wakweli, TFF inazibeba sana timu tatu hizi, na kwa hivyo mojawapo yao haipaswi kulia wivu mwenzake anapobebwa. Sanasana ijiandae kununua ubeleko mpya, maana si aghlabu kwa TFF kutumia ubeleko huohuo mara mbili kuzibebea timu hizi!
Kwaiyo tuwasaidieje na mechi ni jumamos
 
Back
Top Bottom