mkuu ni mara mbili nimeshapata tatizo la Pesa kugoma kutoka kwenye ATM Machine, nilipita kwenye ATM za PBZ hapa Malindi Zanzibar, siku ya kwanza rlinasa 10,000 baada ya wiki 3 ikanasa 40,000, ATM machine ile ile nikaingia mpaka ndani ya Bank sikupata maelezo ya kuridhisha nikawapigia Azania Bank Dar ikawa hakuna maelezo ya kutosha sikuridhika, kwanini ikitokea tatizo kama hii hamuwezi kulishughulikia? Mbona CRDB nilipata tatizo nilipata huduma within 10 Minutes? Inabidi muangalie hayo mabenki mnayoshirikiana nao sio wastaarabu
Uswege utalipia matangazo hapa au bure!hongera kutaka kujua matatizo ya atm zenu ili mziboreshe,biashara ushindani jitahidini sana kuboresha huduma zenu,kama mtaweza washaurini equity bank nao wajiunge na atm zenu!!!!!
kwa kweli nimefarijika leo kukuta hii mada;
Nilifungua akaunt benki ya posta kwa matumaini ya umoja switch,lakini ni shida tu hapa Moshi,karibu matawi yenu yote hapa ni matatizo,hakuna mtandao kila mara na sasa sitaki hata kuweka fedha kwenye akaunt ya posta kwa ni usumbufu mwingine wakati fedha ni zako lakini zinakutesa
Kwanini umoja switch hamuweki features za ku-support visa na master card, ili tusio wateja wa bank zilizopo under umoja switch tuwezw kutumia ATM zenu?
Lingine nikufahamishe kama hujawahi kulisikia, kipindi cha nyuma sera ya BOT ilikuwa ni kuwekeza kwenye ATM Switch moja kwa mabenki yote Tanzania. Na lengo ilikuwa ni kupunguza transaction costs, lakini nasikia baadhi ya banks ....hasa kubwa zilipinga sana suala hili!
safi sana mnajitahidi kutoa huduma nzuri,mi ni mmojawapo wa watumiaji wa huduma zenu,boresheni tu tatizo la networks baadhi ya sehemu other wise keep it up!
Rich Dad,
Visa na MasterCard zipo kwenye mipango yetu, bahati mbaya sio kwenye mipango ya hivi karibuni, it is safe to say, at least not this year. Kila kitu ni project na sasa tunelekeza nguvu kwenye mobile channel, cardless na interbank transactions, hizi zote zitakua live kufika mwezi wa 11 mwaka huu.
Point of correction, BOT walikua wanaongea kuhusu national switch na sio ATM switch, ndio nimewahi kusikia, Labda itakua ni busara zaidi kwa wao kuiendeleza UmojaSwitch (zaidi ya 50% ya mabenki yote tanzania ni wanachama wa umojaswitch) kuliko kuanza switch mpya
discussion hii nzuri, ANGALIZO wana jf msije kujadiliana kuhusu PIN hiyo nenda personally kwenye tawi lako.
Mgeni hufanya vizuri kuja lakini hukaribishwa sebuleni tu.
Iswege,
Kama nimepoteza atm card yangu pamoja na simu, na kwenye simu kuna password (PIN), nitafanyaje haraka aliyeeiba asichukue fedha kwenye akaunti yangu ?
Pole sana manyanza,
- Ulifanikiwa kutatuliwa tatizo lako? kama hapana niandikie kwenye uswege.mwaipyana@umojaswitch.co.tz nitalifatilia
- Tumekusikia na tunajitajidi sasa kuondosha kero kwa wateja wetu, ikitokea unapata shida siku ingine, kama umewasiliana na benki na bado hujaridhika, tafadhali wasiliana na sisi
asante mkuu, sikuwepo humu jamvini baada ya kula BAN, hiyo ya tsh 40,000 nilipata solution, hiyo 10,000 sikupata solution maana niliona ni usumbufu nikaamua kuachana nayo, if possible unaweza kunisaidia mkuu..
ndio inawezekana, nitumie details za hiyo transaction kwenye email yangu.
1. ATM uliyotumia
2. Tarehe uliyoenda
3. Namba ya card (siyo PIN) ila namba hiyo imeandikwa juu ya kadi yako