Athari za ukiukwaji wa sheria ktk kuwawajibisha watumishi wa umma ni kuwadhalilisha watumishi.

HGYTXK

Senior Member
Oct 3, 2011
194
70
Awali nitangulize pongezi zangu kwa dhamira binafsi za raisi JPM na waziri mkuu ktk kufumua uozo ambao kwa kipindi kirefu sana ulionekana ni wivu na propaganda kwa wale waliojaribu kuonyesha na kukemea.
Hojayangu leo ni kuwapa uushauri viongozi hawa wakuu pamoja na serikali kwa ujumla juu ya subira na taratibu ktk kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowahusu watumishi wa umma ambayo yamebatizwa jina la utumbuaji majipu. Ata kama mtumishi kakosea zipo taratibu za kufuata ata zikiwa za muda mfupi lkn sio kumfokea au kumdhalilisha mtumishi mbele ya kadamnasi. Waitwe wahojiwe nata wafokewe ata kama ni kwa siku mzima lkn sio mbele ya watu wanaowahudumia. Kufanya hivyo ni kushusha heshima na morali ya watumishi mbele ya jamii. Matokeo ya haya yanayofanyika yanaanza kuonekana sasa,ukienda bandarini sasa kila raia anajifanya askari kuwafokea watumishi ata kwenye vitu vilivyo nje ya uwezo wao,hii ipo pia tra na kwengineko ambako utumbuaji umeshapita.
Mfano wa karibu zaidi ni huu wa Mtwara ambapo ni wiki kadhaa PM katoka kumsimamisha daktari mbele ya wananchi,jana kumeripotiwa tukio la udharililishaji kwa daktari baada ya baadhi ya wananchi kutoridhishwa na huduma za daktari huyo kwa mgonjwa wao. Ata ndani ya nyumba kama baba na mama hawaonyeshi kutothamini mchango wa dada au kaka wa kazi na kuwadhalilisha mbele ya watoto wao usitegemee watoto watawaheshimu ata kama ni watu muhimu sana kwao maana ndio wanaokaa na familia kwa muda mrefu zaidi kuliko ata hao wazazi.
Ata hivyo watumishi wa umma timizeni wajibu wenu ili kulinda heshima yenu mbele ya jamii na viongozi mtumie sheria,taratibu na busara ktk kuwawajibisha watumishi wanaokiuka maadili.

Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom