Athari za BREXIT kwenye ligi kuu ya England

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,712
5,051
Nchi ya Uingereza imepiga kura ya kujiindoa kwenye umoja wa ulaya EU kujiondoa huko kunaweza kuleta athari kubwa kwa Uingereza katika nyanja mbalimbali ikiwemo mchezo unaopendwa zaidi duniani wa Soka na hususani Ligi kuu ya England.


(i) Baada ya UK kujiondoa kwenye EU, timu za uingereza hazitaweza kusajili tena wachezaji chini ya miaka 16 (under 16) kama ambavyo Manchester United ilifanya katika usajili wa Adnan Januzaj.


(ii) Wachezaji kutoka nchi nyingine za EU zamani hawakuhitaji kibali cha kufanya kazi (work permit) ndani ya uingereza, sasa hivi wote inabidi waanze kutafuta vibali hivyo (work permit)..


(iii) Ukumbuke, na moja ya vigezo vya kukupa kibali cha kufanya kazi ndani ya ardhi ya Uingereza (work permit) ni idadi ya mechi ulizo chezea timu yako ya taifa... kumbuka kuna kukataliwa katika kuomba vibali hivyo..


(iv) Karibu robo tatu kama siyo nusu ya wachezaji wanaocheza ligi kuu ya uingereza (premier league) watahitaji kutafuta vibali vya kufanya kazi (work Permits)ndani ya nchi hiyo...


(v) Zaidi ya wachezaji 100 wataathirika na UK kujitoa kwenye EU, klabu kama Aston Villa, Newcastle United, Watford wataathirika kwa kupoteza wachezaji 11 kutoka kwenye vikosi vyao..


(vi) Klabu ya Charlton Athletic itapaswa kutafuta wachezahi 13 wapya sasa kama mpango huu ukipata kibali rasmi cha UK kujiondoa EU..


(vii) Wachezaji 23 pekee kati ya 180 ambao siyo waingereza, ambao sasa wanacheza kwenye ligi daraja la kwanza (Championship) ndiyo wenye kufikia vigezo vya kufanya kazi ndani ya uingereza..


(viii) Wachezaji 53 ambao wanatoka nje ya uingereza ila nchi zao ni wanachama wa EU, watafanikiwa kucheza ligi kuu ya Uskochi (Scotland) kutokana na kigezo kimoja tu, idadi ya mechi walizocheza na timu zao za taifa..


Hivyo, England kujiondoa kwenye jumuia ya umoja wa ulaya kutakuwa na athari kubwa sana katika soka la nchi hiyo, na linakwenda kuathiri na ligi hiyo kwa kiasi kikubwa sana..


Maamuzi ya kisiasa yanaweza kuathiri ustawi wa soka la uingereza kwa sehemu kubwa sana.. Hata wachezaji wazuri, hawafanikiwa kuingia uingereza kutokana na ugumu wa kupata vibali vya kufanya kazi nchini humo..


Asanteni.


Source..... Wapendasokablog
 
Back
Top Bottom