ATCL ni shirika la Muungano?

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,774
Reaction score
12,084
Wadau, habari zenu

Naomba maoni yenu

Je ATCL ni shirika la Muungano? Nafasi ya Zanzibar ni ipi kwenye biashara ya kukopeshana?, Nijuze kwa wajuwao.

 
Ni shirika ama unaweza sema ni taasisi ya serikali inayojitegemea kujiendesha yenyewe kibiashara kwa manufaa ya waTZ wote bara na visiwani.
Mluguru ruksa,mpemba ruksa,mndengereko ruksa kupanda.Hakuna ubaguzi.CUF,CDM,TLP,ACT,CCM,CHAUMMA,NLD wote wote ruksa kupanda.....ndo raha ya maendeleo..!!Hayachagui !!
 
toafauti na swali lililoulizwa. We unaleta ushabiki usio na maana. Mtoa hoja kahoji je shirika la atcl ni jambo la muungano au sio la muungano? Na kama jibu ni la muungano ipi nafasi ya zanzibar?
 
Kilichoulizwa na jibu lako tofauti kabisa. Enzi za Dada Faiza Foxy alipenda kuuliza shule mlienda kusomea ujinga?
 
ATCL ni zao lililotokana na hisa ya Tanzania bara katika East African Airways baada ya kuvunjika Jumuiya ya Africa Mashariki. Zanzibar ilikuwa mwana Jumuiya na bila shaka ilipata mgao wake.

Hivyo atcl ni mali ya bara peke yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…