Asymetrical chest....

Ze Pro-Money

Member
May 4, 2012
30
6
Kuwa na kifua chenye ukubwa tofauti (yani upande mmoja wa kifua ni mkubwa kuliko mwingine) Nini chanzo chake na je kuna tiba yake? Msaada tafadhali!
 
Mkuu Ze Pro-Money, "Asymetrical chest", kutokuwa na usawa/ulinganifu wa kifua..huweza kusababishwa na mambo mbalimbali zikiwepo
-Magonjwa ya Kurithi.
-Magonjwa ya kuzaliwa nayo.(mf. viungo vikubwa)
-Magonjwa mengi baada ya kuzaliwa( Infections, Kansa, Matibabu-Upasuaji, mitoki, n.k)

Hata hivyo muda wa tatizo(Lilikuwepo/lilianza lini, tabia ya ukuaji wake(homa, kupungua uzito), n.k pamoja na vipimo mbalimbali huweza kusaidia kujua hasa tatizo ni nini.
 
Last edited by a moderator:

Ahsante mkuu. Lakini nataka kufahamu kama tatizo hili ni la kawaida au la, kwa sababu sijapata kusikia likizungumziwa sana!
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu. Lakini nataka kufahamu kama tatizo hili ni la kawaida au la, kwa sababu sijapata kusikia likizungumziwa sana!

Mkuu, Sijui "u-kawaida" unaouongelea ni upi, kati ya haya 1. Hivyo ndivyo kifua kinatakiwa kuwa AU
2. Ukiwa na tatizo hili na halikuletei shida katika maisha yako(shughuli za kila siku)

Pamoja na hayo ningesema kwa"KAWAIDA" kifua kinatakiwa kiwe kwenye ulinganifu(Symmetrical), yaani upande wa kushoto na kulia, upande wa mbele na nyuma, sasa kuna mambo kadhaa ambayo huweza kusababisha kutokuwa na ulinganifu huo.

Mengi kati ya hayo(nilitaja machache tu), huweza kuvumilika na mtu kuishi pasipo tatizo hadi pale mtu huyo atakapovua nguo aliyovaa/kumfunika kifuani.

Bila kutambua mambo kadhaa niliyosema mwanzo ni ngumu kueleza. Ningekushauri kufika hospitalini kwa uchunguzi au kupiga picha eneo lote la kifua(iwapo u mbali na hospitali).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom