Kampuni iliyojipatia umaarufu kwa kutengeneza transformer tablet wamefanya uzinduzi katika maonyesho ya MWC huko Barcelona na kutangaza simu/tablet mbili kwa pamoja. Wakati wengi walitarajia kuwa Asus ingetangaza Padfone mpya lakini hakuna aliyetegemea kwamba sambamba na Padfone hiyo wangetaza Fonepad.
Padfone Infinity ni simu yenye ukubwa wa 5 na imeambatanishwa na tablet dock yenye ukubwa wa 10.1 ambapo unapoiingiza simu hiyo ndani ya dock inakuwa ni tablet kamili. Padfone Infinity ni toleo la tatu katika mfululizo wa familia ya Padfone, ambapo uzuri wake ni kwamba huna haja ya kadi za sim mbili kwa ajili ya tablet na simu.
Kwa ukamilifu na chanzo cha makala hii: http://www.gajetek.com/2013/02/asus-kutoa-padfone-infinity-na-fonepad.html#more