Askofu Thadaeus Ruwa'ichi: 2025 ulikuwa mwaka mgumu na mzito

Askofu Thadaeus Ruwa'ichi: 2025 ulikuwa mwaka mgumu na mzito

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thadaeus Ruwa'ichi amesema 2025 ulikuwa mwaka mgumu na mzito.

Amesema mwaka huo ambao pia ulikuwa Jubilei Kuu, ulikuwa na changamoto hasa kwao kama Watanzania, akisisitiza ulikuwa mgumu, wa majonzi, masikitiko na vifo.

Katika ibada hiyo, Askofu Mkuu Ruwa'ichi alianza kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya waumini akieleza namna binadamu walivyojaaliwa kuzungumza.

Akizungumzia ugumu wa mwaka 2025 na uzito wa mwaka huo, Askofu Ruwa'ichi amesema,"Tukiwa tunanza mwaka mpya, jana usiku tumehitimisha mwaka 2025 mwaka mzito, mzito kwa vipi? kwa sababu ulikuwa ni mwaka wa Jubilei, tumshukuru Mungu ametujaza neema nyingi kama watu binafsi, kama kanisa na kama taifa.

Amenukuu akisema Waswahili husema 'shukuru na kuomba tena', kwa hiyo wanaoshukuru kwa baraka walizopewa wanamuomba Mungu tena awabariki, kuwalinda, kuwabeba katika mikono yake inayoaminika kwa kipindi chote cha mwaka 2026.
1767260561704.png
 
Kiukweli tangu tuingie karne ya 21 mwaka 2025 ndio mwaka mbaya zaidi katika taifa letu kwa sababu ambazo kila mtu anazifahamu.

2025 will go down as the darkest year in our nation.
 
Back
Top Bottom