Askofu Kakobe: Usalama wa Taifa msihangaike nami. Adai kuna kiongozi kavaa hirizi!

Status
Not open for further replies.
Acheni uoga mbona Nabii daniel alipambana na serikali mpaka ikanyooka hadi mfalme Nebuchadnezzar akasalimu amri...... Pia shadrack meshack na abednego walipambana na serikali kisa misimamo ya kidini na serikali ilikuja kusalimu amri

Narudia Tena hakuna serikali ina nguvu zaidi ya Mungu.... Kma Kakobe kweli ana Mungu basi siku mkimgusa ndio mtaelewa nasema nini


zitto junior ,

Hizo za Daniel ilikuwa wakati wa mambo ya agano la kale.

Baada ya Yesu kuzaliwa utendaji wa Mungu ulibadilika.
Siku hizi utubu au unakufa unasubiria hukumu hapo baadae.
 
Amevuka mipaka

Huwezi kuwatisha intelligence service na huenda kwenye kanisa lake kuna mapandikizi ,anaweza kufanywa chochote ni ujuha kuwekeana bifu na kuwatukana tiss mbele ya watu kutafuta sifa
Ni ujuha pia kuwa kama kondoo.
 
Namkumbusha kakobe ogopa kitu kinachoitwa serikali

Serikali yeyote ile duniani haishindwi na kitu ,kujigamba ,kujikweza na ku-provoke usalama wa taifa na kutishia hapa umekengeuka..hekima ni kuchagua maneno sahihi ya kusema

Chunga mdomo wako huwezi kushindana na serikali yeyote ile duniani ,utajipoteza tu mifano ipo mingi


Sipingi kukosoa napinga vitisho na kujikweza alizotoa Askofu


Hao usalama wa taifa anaowatisha wanaweza kumuwekea zengwe akafukuzwa nchini ,majamaa wana style tofauti tofauti

Ni ujinga kuwekeana bifu na intelligence ss

Acha woga
 
Huyu alishafika keko? nadhani tatizo sio kakobe tatizo wanaotuletea maneno yake.
 
Rai yangu Serikali kutaneni na Viongozi wa Dini zetu. Zungumzeni vizuri huku mkitambua wajibu mkubwa sana mlionao kwenye jamii. Watendeeni haki watanzania ili tuendelee kuishi kwa Amani na Utulivu. Majibizano na mtifuano kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii hayana mshindi bali ni kuvurugana tu
 
Hakuna wa Kushindana na Mungu.

Hakuna aliyeshindana na watu wa Mungu na akashinda tangu kuwekwa misingi ya Dunia.
Hallelujah!!ni neno moja tam sana kulisema pale unapoona kiumbe lilicho umbwa na Mungu kinampa Mungu sifa zake zoote.ina kuwa hallelujah kwa Bwana.

~Pamoja na mizaha yetu humu ndani kumbe Mungu ana nafasi kubwa sana kwetu,hasa pale tunapo amini kuwa yupo na anaweza.imani si tu kwa tulio okoka hata ambao bado wakiamin kwa Mungu wana barikiwa sawasawa na imani yao japo ni nje ya hema.

~Acha Mungu ajitetee kwa ajili ya jina lake mwenyewe.
 
anaheshim utawala wa serikali ndiye atakuwa anaheshim Mungu anayemtumikia ,maana au kwa maana serikali popote duniani kichwa chake Mungu baba , hata biblia inasema heshimuni mamlaka.
 
Ndugu,

Kawatishie unaoweza kufulu kuwatisha.

Kumbuka kwenye dini ndiko kuna jibu kwamba binadamu amekuja vipi hapa duniani na akiondoka hapa duniani anakwenda wapi.

Kikundi unachokiita usalama wa taifa wa taifa lolote hauna majibu hayo na hivyo ni upumbavu kuogopa vikundi vya namna hiyo hasa pale pasipostahili na ndiyo maana kwenye masuala ya dini hakuna usalama wa taifa uliwahi kuogopwa hapa duniani.


Na hili la kutoogopa usalama wa taifa alilisimika Yesu mwenyewe na hata pale Getsemani yule YUda ISkariote alituma na uaslama wa taifa kumsaliti, unaonaje kifo cha Yuda?

Kutoogopa majeshi, polisi na usalama wa taifa ndiko kumefanya ukristo ukashamiri, sasa itashangaza eti vinchi vya dunia ya tatu ambavyo havijatimiza hata miaka 60 vifanye maajabu ambayo dunia hijawahi kuyaona eti viongozi wa dini waogope kuhubiri.

Mfano mwingine ni wa Yohane mbatizaji ambaye usalama wa taifa ulimkata kichwa kwa sababu alimkemea mfalme. Je, manabii walikoma kukemea uovu?

Hivyo, unatwanga maji kwenye kinu kudhani kwamba viongozi wa dini watatishwa na kikundi kama hicho.

Kama Kakobe, Pengo, GWajima, NiweMugizi kakosea lete kosa la hoja yake tukuunge mkono.

Kumbuka kwenye dini humtishi mtu kuuawa kwani wako wengi wamejitolea kufa ili kulidna imani yao. Imani yao ndiyo risasi zao.

Nakushauri kitu kimoja, waambie jamaa zako wabomoe hoja za viongoi wa dini, inatosha. Hakuna aliyewahi kushindana na dini hapa duniani kama dini ikiamua kupambana naye.

Ndiyo maana nimetoa mfano wa Napoleon na nigeweza kutoa mfano wa Hitler na wakomunisto wote.

Ushindwe katika jina la Yesu.

SubiriJibu ,
Mkuu,
Kwanza siamini katika vitabu vya kuletwa na wazungu na warabu kuwa ndizo dini. Hapo kwanza, tuelewane vizuri.

Pili, Naamini katika sanyansi tu " sanyansi naona vitu dhahiri na siyo hadithi za wazungu na warabu .

Tatu, Naamini katika kufanya kazi kwa weredi, juhudi , maarifa, kujituma na nguvu ndiyo mafanikio huja.

Nne, naheshimu Katiba ya Tanzania au sheria za nchi yoyote ile ninapo kwenda kikazi au mapumziko.

Mfano, niko South Africa, mapumziko na familia yangu naheshimu taratibu na sheria za nchi hii huku na siyo dini na madhehebu ya wazungu na warabu na vitabu vyao vya kuleta na majahazi na meli eti ndiyo Mungu..

Hivyo, yeyote anaye tumia vitabu na tamaduni za maisha ya wazungu na warabu hapo Tanzania kinyume na taratibu hasa ukifika kwenye hatua ya kugusa realism theory " UwT " basi unakuwa unaanza kujiita mwenyewe kuingia ndani ya futi sita.

Naomba niishie hapo maana, sayansi na vitabu vya kuletwa havina uhusiano.
 
Naam tulisema tukapuuzwa kama CCM haijui sasa imeingia vitani
VITA YA IMANI NA ITIKADI.
Iko tofauti kubwa CCM kupambana na CHADEMA,CUF,NCCR. ni rahisi kuwatambua maadui wa kiitikadi lakini sio wa kiimani.
Hivi kuna shida gani kujishusha na kutubu au la kaeni kimya acheni vitisho.
Kweli khabisa..! Maana hata Ndani ya CCM kwenyewe kuna Waumini Wanatazama tu huu Mchezo..!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
AO WATUMISH SIJUI NINI NAO AKILI AWANA ET NANI ATAKUJA KUSAL APA KAKOBE AKIONDOKA NAYO YANASEMA HAKUNAAAA ..SASA UYO KAKOMBE NDO MUNGU WENU AU KWAMBA AKIONDOK YEYE UKIENDA KUSALI APO AMNA UTAKACHOKIPATA AU
 
Dah Kakobe anasema amekutana wiki 2 ana kwa ana na Yesu akimpa maagizo usiku na mchana Du huyu jamaa sasa anawapeleka kubaya
 
Kuwapumbaza wapumbavu. Huoni wachangiaji hili swala hawataki kuhoji kuwa ni clip ya lini? Kilichobakia ni kueneza propaganda chafu tu.
Nimewaambia clip hii ya zamani lakini wanaendelea tu kuchonga blindly. Hapo naonana wana bad intention sawa na aliyeiweka. Nijuavyo mimi kila jambo lina majira yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom