Askofu Judae Ruwai’chi azungumzia hali ya siasa nchini

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
375
510
KUTOKANA na hali ya kisiasa nchini ilivyo sasa pamoja na mjadala wa Bunge kupamba moto huku baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakitimuliwa ndani ya Bunge kwa madai ya kukiuka kanuni, Mwandishi Wetu alifanya mahojiano na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Judae Ruwai'chi ili kuweza kupata msimamo wake kuhusiana na hali hiyo pamoja na masuala mengine. Yafuatayo ni mahojiano baina yake na Askofu huyo.


Mwananchi Jumapili: Mhashamu Askofu Mkuu, ukiwa kama kiongozi wa dini unajukumu la kufuatilia na kujua hali ya kisiasa nchini, kwa sasa katika bunge letu tumeshuhudia mambo mengi ikiwa ni pamoja na baadhi ya wabunge Kutimliwa nje ya Bunge, sijui hili unalizungumziaje, unadhani ni kukua kwa Demokrasia?

Askofu Mkuu:
Taifa lipo katika kipindi cha mpito cha kisiasa, na kila taifa linakuwa na historia yake ya kisiasa, kwa upande wa Taifa la Tanzania lilipitia katika ukoloni na mara baada ya uhuru tulionja mazingira ya utawala wa chama kimoja, ambachi kilinawili wakati ulimwengu ulikuwa ukitawaliwa na kambi mbili kubwa za magharibi na mashariki.

Hizo kambi kwa sehemu kubwa zimepitwa na wakati, na sasa huu ulimwengu tunaoishi unaonekana zaidi ni ulimwengu kijiji, kufa kwa kambi za magharibi na mashariki kulisababisha kutokea mambo ambayo yanawapa watu changamoto za mahusiano na utendaji wao.
Hili ni suala ambalo linatakiwa kufanyiwa utafiki wa kina ili wananchi waelewe mwendo wa siasa na uchumi duaniani, hilo pia tulione jinsi linavyojitafsiri katika mazingira yetu ya Tanzania.

Kwa karibu muongo sasa taifa limetoka katika huo muongo wa utawala wa chama kimoja, tukaingia katika awamu ya siasa ya vyama vingi, kuingia katika siasa ya vyama vingi ni safari ambayo inahitaji uelewa, utayari na kuondokana na ukale, mazoea hata matamanio ya namna ya kutenda. Sidhani kwamba yote ambayo yanapaswa kufanyika ili wananchi waelewe kuhusu mfumo wa vyama vingi na namna mfumo huo unavyopaswa kwenda.

Wengi, hili linawahusu watanzania wengi, wako katika mfumo huu lakini wakisukumwa na fikra na muono wa nchi kuwa katika mfumo wa siasa ni za chama kimoja.

Mwananchi Jumapili:
Unaposema hivyo unamaanisha nini baba Askofu?

Askofu Mkuu:
Naomba kuweka bayana, tukitaka kupiga hatua ni lazima tukubali haya yafuatayo, kwamba Tanzania ni nchi ya vyama vingi na hili siyo lakujadili leo ni ukweli, lakini pia Tanzania kuwa nchi ya vyama vingi siyo kosa ni mojawapo ya mpangilio wa kisiasa ambao kwanza unawapa wananchii fursa ya kuchagua na pili unaipa serikali changamoto ya kuwajibika.

Katika utawala chama kimoja watu wanaweza wakajifanyia mambo yao jinsi wanavyotaka bila ya kujua kwamba kuna mbadala, lakini katika vyama vingi kila anayekuwa katika serikal ni lazima atambue kunaweza kuwa na mbadala, hili ni bora kwa raia wote lakini pia kwa vyama vya siasa.

Lakini chama cha siasa kinaweza kufikiri hakuna mbadala basi kinaweza kujiruhusu na kustawisha maotea mabovu ndani yake, ambayo ni kama kansa yanakitafuna chama hicho, lakini kikikumbuka kwamba kuna mbadala kitajiwekea check and balanceses, haya ninayosema nataka kusema kuwa nayasema kwa vyama vyote kwa sababu wale watu ambao wanasikiliza juu juu wanaweza wakazuka na kusema kwamba Askofu mkuu amekilenga chama fulani, ukweli ninaousema unaweza kutumika popote duaniani kwenye mazingira yanayovihusisha vyama.

Haya nilyosema yanajidhihirisha hata katika namna Bunge letu linavyofanya kazi, lakini kabla ya kuzungumzia bunge nivitazame vyombo vya dola kwa ujumla, vyombo vya dola hivi, nataka nivitazame hasa vifuatavyo, Bunge, Mahakama na Serikali.

Hivi ni vitengo vya dola ambavyo, hakuna kimoja ambacho kinaweza kusema kinazidi kingine, vinapaswa kufanya kazi kwa upeo kwa uwajibikaji na ukereketwa wa kitaifa ambao unakuwa na kuwajibishana.

Napenda nijiulize katika mazingira yetu, je, ni kweli vyombo hivi katika mahusiani yake, vimefikia ukomavu wa kutenda kwa uwajibikaji na pili kuwajibishana?

Ninaogopa kwamba hapa kuna bado safari ambayo inatupasa tuifanyie kazi, hivyo kwamba Bunge na wabunge wafanye kazi kama chombo ambacho kinabeba dhamana ya taifa, siyo dhamana ya chama au vyama.

Chama au Vyama ni kama jiwe ambalo mbunge anakanyaga kusudi avuke aingie katika huo ulingo unaoitwa bunge, lakini anaemtuma kule, wanawapeleka kule mwisho wa yote siyo chama ni wananchi wanao piga kura.

Tungependa tufike mahali tuamini, nisisitize hili tuamini, kwamba wanaokuwa Bungeni kweli wanabeba dhamana ya Taifa letu, changamoto za Taifa letu, matamanio ya watu wetu, haki za watu wetu na maslai ya watu wote.

Mara nyingine ukisikiliza majadiliano na namna ya kuendesha unaona kwamba zipo nafasi ambapo watu wanaonyesha kwamba wapo pale pengine wakifikiria maslai yao binafsi, au kama siyo yao binafsi ni ya kikundi hata kama kikundi hicho ni chama.

Lakini Taifa hili halitanawili kwa wale wamechaguliwa na wananchi kwenda kushuhgulikia maslai yao binafsi au maslai ya kikundi fulani, kiwe kikundi cha matajiri au kikundi cha dini, kiwe ni kikundi cha kabila, kiwe ni kikindi cha chama, haliwezi kunawili.

Kwa hiyo hili ninalosema lichukuliwe kama ni assessment ya mtu aliye interest namwenendo wa Bunge na kwa bahati ninaweza kuchambua hivyo, na ni haki yangu ya msingi kikatiba. Yake yaliyojiri katika hili bunge tangu bunge jipya lichaguliwe yanaelekea kujibiwa na hayo niliyoeleza.

Mwananchi Jumapili:
Kuna baadhi ya wanasiasa na Viongozi wakongwe wa serikali na chama cha mapinduzi wanadai kuwa haya yanayotokea leo hapa nchini hususan katika siasa ni mwelekeo wa watu kusaka Urais 2015, wewe unalionaje?

Askofu Mkuu:
Kama kuna mambo yanatokea leo yakiwa yanafungamanishwa na serikali iliyopo au bunge lililopo ama chama kinacho tawala, hayawezi yakatafsiriwa kwa usahihi bila kufikiria historia ya nchi yetu, chama kinachotawala na vyama vingine vilivyopo, na pia historia ya wale ambao wamekabidhiwa majukumu ya kutuongoza.

Mwananchi Jumapili:
Kuna hili la viongozi wa dini kutajwa na Rais kuwa wanajihusisha na madawa ya kulevya, nini maoni yako?

Askofu Mkuu:
Kwanza niliweke katika mazingira yanayoeleweka, kauli ya kuwashutumu viongozi wa dini kwamba wanajihusisha na madawa ya kulevya ilitolewa na rais Kikwete kule Songea wakati wa Jubilee ya Askofu Mkuu Norbert Mtega.

Shutuna ile kwanza nieleze sikuona Busara yake, hapakuwa mahali pake kutoa shutuma kama ile, sababu shutuma kama ile inapoteolewa pale ni kama kuwapaka matope maaskofu waliokuwa pale kwa shutuma zinazosemwa.

Sidhani kama kuna askofu ama padre aliyekamatwa kwa shutuma hizo zilizotajwa, kiongozi wa nchi anapotoa shutuma kama zile ni lazima aamue mahali pa kuzitoa, namna ya kuzitoa na jinsi ya kuzifanyia kazi.

Kama kuna viongozi wanaojihusisha na madawa ya kulevya, hilo linajulikana ni kosa la jinai lisilokubalika kwa sababu linaharibu raia wa nchi hii, ndiyo kusema kwamba ni watu wanaojitajirisha harakaharaka kwa kutumia migongo ya watu fukara wa Taifa hili na kwa sababu hiyo serikali inalojukumu la kulifanyia kazi kwa kutumia nguvu ya sheria na utaratibu wa kisheria.

Sasa kama Rais anajua viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya, tunapenda kumtia moyo kwamba aviwezeshe vyombo vya sheria kuwashughulikia.

Lakini pia niseme yoyote yule anayejihususha na madawa ya kulevya, awe kiongozi wa dini au raia wa kawaida ni lazima ihakikishwe kwamba vyombo vya dola havisaidia uhuni huo, manake haiwezekani nchi yetu ifikiriwe kuwa ni daraja la kuvushia madawa ya kulevya.

Katika nchi za Afrika leo hii Tanzania inafikiliwa kuwa ni kituo muhimu cha kuvushia madawa ya kulevya, vyombo vyetu vya sheria vinavyopaswa kusimamia jambo hilo viko wapi, je serikali yetu imekatwa mikono?

Mwananchi Jumapili:
Serikali imesema na kuwataja viongozi wa dini, haudhani kuwa imetenda?

Askofu Mkuu:
Serikali haipaswi kutenda kwa kusema, shutuma hizo ziwekwe sawa na tatizo la madawa ya kulevya lishughulikiwe kwa utayari, uwazi na uwajibikaji unaoaminika.

Mwananchi Jumapili:
Kuna haya madai ya kuwepo kwa udini, ukiwa kama kiongozi wa Dini, Je, unadhani Tanzania imeingia katika Udini?

Askofu Mkuu:
Kwenye ngazi fulani, na niseme kwamba, kama tunatatizo la udini, hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa wetu. Niseme tu wazi, wanasiasa ambao wametumia njia hiyo lengo lao lilikuwa ni kuwaogopesha watu na kuwarubuni kusudi watu wakighafirika waendele kuwakumbatia.

Tunajua kwamba kuna watu wamezunguka nchi hii wakiimba hiyo ngojera ya udini, wakitetea chama fulani, tumehoji na kusema chama kinachopigiwa debe na dini inayopigiwa debe vimeshakuwa pete na kidole?

Mwisho.
 

Attachments

  • PICT0539.JPG
    PICT0539.JPG
    641.9 KB · Views: 89
Majibu mazuri, ya uwazi bila kumumunya! Honest and candid, Asante sana Baba Askofu, na asante sana uliyeleta hii thread, nimeipenda sana
 
Kile kikundi cha AL SHABAAB :- FaizaFoxy, Ritz, Malaria sugu, sokomo nk mnakaribishwa kuyadadavua mahojiano hayo!
 
Yes Bishop has said it. Inaonekana ameenda shule kwa jinsi anavyojibu hoja.
 
elimu nzuri ndugu zanguni.wapelekeni watoto wenu shule wawe na akili kama za huyo askofu.msg sent.
 
Kweli kabisa askfu huyo anastaili pongezi kwa mchango wake, ni bora mchango wake ukafanyiwa kazi hasa wenzetu wale wanaojivua gamba.
 
Anaitwa Yudas Tadei Rwaichi,alianzia alipoteuliwa jimbo la Mbulu alipoteuliwa kuwa askofu kwa mara ya kwanza,akapelekwa Dodoma, sasa yupo jimbo la Mwanza

Kwa ujumla ni kichwa kinachobeba vyote!
 
Asante sana Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Hapo umenena umetoa hoja zilizoenda shule kama ungekuwa ndo Rais hivi basi bwana wewe ni mtumishi wa Mungu. Lakini umewapa somo waache kuropoka Has Mkuu wetu huyo anongea mambo makubwa kama rais lakini hana ushahidi. Halafu anaongea mahali pasipo husika. Tujifunze kuongea kitu sahihi kwa wakati sahihi na mahali sahihi siyo bora kimekuja kichwani. MESSAGE SENT AND I AM SURE IT HAS BEEN DERIVED.
 
Asante sana Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Hapo umenena umetoa hoja zilizoenda shule kama ungekuwa ndo Rais hivi basi bwana wewe ni mtumishi wa Mungu. Lakini umewapa somo waache kuropoka Has Mkuu wetu huyo anongea mambo makubwa kama rais lakini hana ushahidi. Halafu anaongea mahali pasipo husika. Tujifunze kuongea kitu sahihi kwa wakati sahihi na mahali sahihi siyo bora kimekuja kichwani. MESSAGE SENT AND I AM SURE IT HAS BEEN DERIVED.
hapo kwenye red vipi? ila ujumbe umefika!
 
Yes Bishop has said it. Inaonekana ameenda shule kwa jinsi anavyojibu hoja.
Of course jamaa kaenda shuleni.Mimi nilimuona akiongea live Singida miaka ya 2007 ,nilipenda jamaa anavyoongea kimantiki ,kwanza jamaa na maconfidence ya ajabu,kwa nini?kaenda shule zimo kichwani. Wale mnaopenda kudadavua kila mahali semeni sasa!!!!!!!!!!!
 
It's a very interesting conversation! Naamini kwa kiongozi yeyote yule aliyeiva,hasa kiongozi wa dini yeyote inayoamini katika kusema ukweli, ukizungumza naye utapata uzito fulani wa hoja,busara na unyenyekevu fulani ambao huja tu kwa miaka mingi ya kujifunza(sio tu kusoma) na kujitiisha(discipline).

Bishop Rwaichi(also president of the TEC), amenifikirisha sana hasa katika mtizamo wa 'mbadala' unaopaswa kuja na dhana ya vyama vingi na mabadiliko ya fikra za watu kwa wakati huu, kuacha kutegemea bunge na siasa kwa ujumla kuendeshwa kama wakati wa chama kimoja. It is obvious that the CCM mp's who constantly oppose CHADEMA's way of doing things in parliament or outside (especially the demos), are living in the past! Ndungai,Makinda and other seat chairers, STOP DWELLING IN THE PAST!..cos a new moon has risen.
 
Back
Top Bottom