Askofu amwangukia Magufuli, Amtaka asiwatumbue misamaha ya kodi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
ASKOFU wa Kanisa la Anglikani nchini (KAT), Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Askofu Stanley Hotay, amesema kanisa halina majipu ya kutumbuliwa kwa kuwa linatoa huduma zinazoisaidia Serikali kupeleka maendeleo kwa Watanzania.

Kauli ya Askofu Hotay aliyoitoa mjini hapa jana wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid imekuja wakati mwenendo wa uongozi wa Rais John Magufuli ni wa kutumbua majipu kutokana na kile alichokisema Februari, mwaka huu wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam kuwa alikuta uozo mkubwa serikalini.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, Askofu Hotay alipongeza juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Magufuli.

Askofu Hotay ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Kanisa la Arusha alisema kumekuwapo na taarifa
za waraka wa kuondolewa kwa misamaha ya kodi kwa kanisa hatua aliyosema kama itatekelezwa itarudisha nyuma
juhudi za kuisaidia Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tunakuomba mkuu wa mkoa utusaidie kufikisha hili. Lakini pia liangaliwe vizuri sisi hatuna majipu kabisa.
Tunasaidiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii,” alisema Askofu Hotay.

Kwa upande wake, Ntibenda, aliwaomba viongozi wa kanisa kuisaidia Serikali kuhamasisha vijana kufanya
kazi.
“Rais Magufuli amenipa majukumu ya kuhakikisha watu wanafanya kazi hasa vijana badala ya kucheza mchezo wa pool.

Tabia hii ikiachwa itatengeneza Taifa la wavivu na walalamikaji,” alisema Ntibenda.
Alisema Serikali itaendeleza ushirikiano uliopo baina yake na taasisi za dini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu
wake wanaendelea kuabudu kwa amani na utulivu.

Katika ibada hiyo, Ntibenda, alilazimika kutoa namba yake ya simu ambayo ni 0766030000 na 0754604003
baada ya kuwataka wananchi wasikubali kutoa rushwa katika maeneo ya huduma za kijamii.

“Nawaomba wananchi nipigieni simu pindi mnapoombwa rushwa katika huduma za kijamii na maeneo mengine.
Nisaidieni kupambana na vita hii,” alisema Ntibenda ambaye namba yake ilisomwa kwa wananchi na Askofu Hotay.

MAGUFULI

Kwa upande wake, Rais Magufuli, aliwashangaza waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililoko Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kusimamisha msafara wake na kisha kusalimiana na walemavu.

Tukio hilo lilitokea jana katika lango la kutokea kanisani hapo ambako alikwenda kuhudhuria Ibada ya Ijumaa
Kuu.
Magufuli alifika kanisani hapo mapema na kusali pamoja na waumini wa kanisa hilo na ibada ilipoisha alipanda katika gari lake na kuondoka.

Wakati akiondoka alikuwa akiwapungia mkono waumini hao na alipofika langoni hapo ghafla msafara wake ulisimama na kisha kushuka ili kuwasalimia waumini hao jambo lililowafanya wengine kusogea
ili kujua kilichotokea.

Magufuli alishuka na kuwafuata walemavu waliokuwa wamekaa jirani na lango hilo la kutokea na kuzungumza
nao.
Ingawa mazungumzo hayo hayakusikika, kitendo cha kushuka na kuzungumza na walemavu hao kiliwafanya watu waliokuwapo jirani na eneo hilo kuvutiwa na alipomaliza alipanda tena katika gari yake na msafara huo kuondoka kuelekea Ikulu.

Awali, akizungumza katika mahubiri hayo, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Stephano Kaombwe, aliwasihi
Watanzania kuwa na moyo wa upendo.

Huku akinukuu katika Biblia Takatifu katika injili ya Yohana, Kaombwe alisema inashangaza kwamba Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya wanadamu lakini wenyewe bado
wanachukiana.

“Wanadamu hatukuumbwa tuteseke, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona Mungu aliwaweka Adam na
Hawa kwenye bustani ili waishi vizuri, wastarehe lakini walitenda uasi,” alisema Kaombwe.

Chanzo Mtanzania

maoni yangu

viongozi wa dini nao wanapaswa kuwa wakweli, wengine wanatumiwa na wafanyabiashara katika kuingiza vifaa vyao kama magari nk kutumia misikiti na makanisa kwa nia ya kukwepa kodi ambayo inaikosesha serikali mapato.

pili wapunguze gharama za hospital zimekuwa na gharam kubwa mpaka zinaleta mshangao, unakuta gharama zipo juu zaidi ya hata hospital binafsi wakati wao wanapata msamaha.
 
Ni kweli ayasemayo.

Hakuna majipu kanisani.

1. Wamejenga shule zinatoa elimu bora,
2. Wamejenga vyuo vikuu vinavyotoa elimu bora,
3. Wamejenga mahospitali yaliyogeuka mbadala wa hospitali za Rufaa za serikali,
4. Misaada ya kijamii, kulea yatima, wajane nk,
5. Mwisho kabisa, Kuleta HOFU ya MUNGU kwa watu na kujenga jamii yenye upendo na umoja...
 
Bure au wanafanya biashara?
 
Sifa za magufuli zimepitiliza amaenza sasa anawafanyia utani viongozi wa dini hivi Magufuli sasa yuko juu ya huduma za Mungu ajabu kweli
 
ASKOFU wa Kanisa la Anglikani nchini (KAT), Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Askofu Stanley Hotay, amesema kanisa halina majipu ya kutumbuliwa kwa kuwa linatoa huduma zinazoisaidia Serikali kupeleka maendeleo kwa Watanzania.

Kauli ya Askofu Hotay aliyoitoa mjini hapa jana wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid imekuja wakati mwenendo wa uongozi wa Rais John Magufuli ni wa kutumbua majipu kutokana na kile alichokisema Februari, mwaka huu wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam kuwa alikuta uozo mkubwa serikalini.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, Askofu Hotay alipongeza juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Magufuli.

Askofu Hotay ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Kanisa la Arusha alisema kumekuwapo na taarifa
za waraka wa kuondolewa kwa misamaha ya kodi kwa kanisa hatua aliyosema kama itatekelezwa itarudisha nyuma
juhudi za kuisaidia Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tunakuomba mkuu wa mkoa utusaidie kufikisha hili. Lakini pia liangaliwe vizuri sisi hatuna majipu kabisa.
Tunasaidiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii,” alisema Askofu Hotay.

Kwa upande wake, Ntibenda, aliwaomba viongozi wa kanisa kuisaidia Serikali kuhamasisha vijana kufanya
kazi.
“Rais Magufuli amenipa majukumu ya kuhakikisha watu wanafanya kazi hasa vijana badala ya kucheza mchezo wa pool.

Tabia hii ikiachwa itatengeneza Taifa la wavivu na walalamikaji,” alisema Ntibenda.
Alisema Serikali itaendeleza ushirikiano uliopo baina yake na taasisi za dini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu
wake wanaendelea kuabudu kwa amani na utulivu.

Katika ibada hiyo, Ntibenda, alilazimika kutoa namba yake ya simu ambayo ni 0766030000 na 0754604003
baada ya kuwataka wananchi wasikubali kutoa rushwa katika maeneo ya huduma za kijamii.

“Nawaomba wananchi nipigieni simu pindi mnapoombwa rushwa katika huduma za kijamii na maeneo mengine.
Nisaidieni kupambana na vita hii,” alisema Ntibenda ambaye namba yake ilisomwa kwa wananchi na Askofu Hotay.

MAGUFULI

Kwa upande wake, Rais Magufuli, aliwashangaza waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililoko Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kusimamisha msafara wake na kisha kusalimiana na walemavu.

Tukio hilo lilitokea jana katika lango la kutokea kanisani hapo ambako alikwenda kuhudhuria Ibada ya Ijumaa
Kuu.
Magufuli alifika kanisani hapo mapema na kusali pamoja na waumini wa kanisa hilo na ibada ilipoisha alipanda katika gari lake na kuondoka.

Wakati akiondoka alikuwa akiwapungia mkono waumini hao na alipofika langoni hapo ghafla msafara wake ulisimama na kisha kushuka ili kuwasalimia waumini hao jambo lililowafanya wengine kusogea
ili kujua kilichotokea.

Magufuli alishuka na kuwafuata walemavu waliokuwa wamekaa jirani na lango hilo la kutokea na kuzungumza
nao.
Ingawa mazungumzo hayo hayakusikika, kitendo cha kushuka na kuzungumza na walemavu hao kiliwafanya watu waliokuwapo jirani na eneo hilo kuvutiwa na alipomaliza alipanda tena katika gari yake na msafara huo kuondoka kuelekea Ikulu.

Awali, akizungumza katika mahubiri hayo, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Stephano Kaombwe, aliwasihi
Watanzania kuwa na moyo wa upendo.

Huku akinukuu katika Biblia Takatifu katika injili ya Yohana, Kaombwe alisema inashangaza kwamba Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya wanadamu lakini wenyewe bado
wanachukiana.

“Wanadamu hatukuumbwa tuteseke, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona Mungu aliwaweka Adam na
Hawa kwenye bustani ili waishi vizuri, wastarehe lakini walitenda uasi,” alisema Kaombwe.

Chanzo Mtanzania

maoni yangu

viongozi wa dini nao wanapaswa kuwa wakweli, wengine wanatumiwa na wafanyabiashara katika kuingiza vifaa vyao kama magari nk kutumia misikiti na makanisa kwa nia ya kukwepa kodi ambayo inaikosesha serikali mapato.

pili wapunguze gharama za hospital zimekuwa na gharam kubwa mpaka zinaleta mshangao, unakuta gharama zipo juu zaidi ya hata hospital binafsi wakati wao wanapata msamaha.
Mimi napinga kile kinachoitwa HATUA YA KUISAIDIA SERIKALI. HUU NI UONGO. Serikali haiwezi kusaidiwa. JPM futa misamaha yote ya kodi. Bei za huduma ni ghali mno,halafu tunaambiwa eti ni KUISAIDIA SERIKALI. Futa misamaha yote, watu walipie huduma stahiki ikiwa kodi tayari ishakatwa. Hiyo iwe ni kwa taasisi ZOTE za DINI na wadau wengine wanaokuja kwa mgongo wa NGO
 
askofu SHOO yeye alishangaa serikali kutumbua watoa sadaka wake wakiongozwa na mbowe
 
Kwa dini zote,ile tabia ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi Kwa kutumia taasisi za kidini kuingiza bidhaa nchini ikome mara moja.
Serikali hii iko makini kufuatilia mienendo ya hizi taasisi.
Auditing.
 
ASKOFU wa Kanisa la Anglikani nchini (KAT), Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Askofu Stanley Hotay, amesema kanisa halina majipu ya kutumbuliwa kwa kuwa linatoa huduma zinazoisaidia Serikali kupeleka maendeleo kwa Watanzania.

Kauli ya Askofu Hotay aliyoitoa mjini hapa jana wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid imekuja wakati mwenendo wa uongozi wa Rais John Magufuli ni wa kutumbua majipu kutokana na kile alichokisema Februari, mwaka huu wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam kuwa alikuta uozo mkubwa serikalini.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, Askofu Hotay alipongeza juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Magufuli.

Askofu Hotay ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Kanisa la Arusha alisema kumekuwapo na taarifa
za waraka wa kuondolewa kwa misamaha ya kodi kwa kanisa hatua aliyosema kama itatekelezwa itarudisha nyuma
juhudi za kuisaidia Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tunakuomba mkuu wa mkoa utusaidie kufikisha hili. Lakini pia liangaliwe vizuri sisi hatuna majipu kabisa.
Tunasaidiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii,” alisema Askofu Hotay.

Kwa upande wake, Ntibenda, aliwaomba viongozi wa kanisa kuisaidia Serikali kuhamasisha vijana kufanya
kazi.
“Rais Magufuli amenipa majukumu ya kuhakikisha watu wanafanya kazi hasa vijana badala ya kucheza mchezo wa pool.

Tabia hii ikiachwa itatengeneza Taifa la wavivu na walalamikaji,” alisema Ntibenda.
Alisema Serikali itaendeleza ushirikiano uliopo baina yake na taasisi za dini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu
wake wanaendelea kuabudu kwa amani na utulivu.

Katika ibada hiyo, Ntibenda, alilazimika kutoa namba yake ya simu ambayo ni 0766030000 na 0754604003
baada ya kuwataka wananchi wasikubali kutoa rushwa katika maeneo ya huduma za kijamii.

“Nawaomba wananchi nipigieni simu pindi mnapoombwa rushwa katika huduma za kijamii na maeneo mengine.
Nisaidieni kupambana na vita hii,” alisema Ntibenda ambaye namba yake ilisomwa kwa wananchi na Askofu Hotay.

MAGUFULI

Kwa upande wake, Rais Magufuli, aliwashangaza waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililoko Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kusimamisha msafara wake na kisha kusalimiana na walemavu.

Tukio hilo lilitokea jana katika lango la kutokea kanisani hapo ambako alikwenda kuhudhuria Ibada ya Ijumaa
Kuu.
Magufuli alifika kanisani hapo mapema na kusali pamoja na waumini wa kanisa hilo na ibada ilipoisha alipanda katika gari lake na kuondoka.

Wakati akiondoka alikuwa akiwapungia mkono waumini hao na alipofika langoni hapo ghafla msafara wake ulisimama na kisha kushuka ili kuwasalimia waumini hao jambo lililowafanya wengine kusogea
ili kujua kilichotokea.

Magufuli alishuka na kuwafuata walemavu waliokuwa wamekaa jirani na lango hilo la kutokea na kuzungumza
nao.
Ingawa mazungumzo hayo hayakusikika, kitendo cha kushuka na kuzungumza na walemavu hao kiliwafanya watu waliokuwapo jirani na eneo hilo kuvutiwa na alipomaliza alipanda tena katika gari yake na msafara huo kuondoka kuelekea Ikulu.

Awali, akizungumza katika mahubiri hayo, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Stephano Kaombwe, aliwasihi
Watanzania kuwa na moyo wa upendo.

Huku akinukuu katika Biblia Takatifu katika injili ya Yohana, Kaombwe alisema inashangaza kwamba Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya wanadamu lakini wenyewe bado
wanachukiana.

“Wanadamu hatukuumbwa tuteseke, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona Mungu aliwaweka Adam na
Hawa kwenye bustani ili waishi vizuri, wastarehe lakini walitenda uasi,” alisema Kaombwe.

Chanzo Mtanzania

maoni yangu

viongozi wa dini nao wanapaswa kuwa wakweli, wengine wanatumiwa na wafanyabiashara katika kuingiza vifaa vyao kama magari nk kutumia misikiti na makanisa kwa nia ya kukwepa kodi ambayo inaikosesha serikali mapato.

pili wapunguze gharama za hospital zimekuwa na gharam kubwa mpaka zinaleta mshangao, unakuta gharama zipo juu zaidi ya hata hospital binafsi wakati wao wanapata msamaha.
Hivi wewe huoni aibu?post ina masaa 9 wachangiaji 8 tu?ujue ndio umepost kituko na watu wameisusia
 
Back
Top Bottom