Habari wakuu,
Jana jion saa 11 nilenda bagamoyo kwenye mualiko wa futari bahati mbaya nilivyofika mapinga nilisimamishwa na trafiki kwa kosa la kuendesha gari zaidi ya km 50 kwa saa, sikupinga huo uamuzi ila niliwaomba waniandikie notification ili nikailipe kesho maana sikuwa na hela cash kwa muda huo kimbembe kikaanzia hapo.
Trafiki hawataki nikalipie sehem nyingine na wanataka nilipe hapo hapo na kusema utaratibu wa efd au kulipa siku nyingine ni kwa dar pekee huku nikipewa na vitisho kuwa nisipolipa hiyo faini papo hapo nipeleke gari kituoni hadi nitakapoleta hiyo hela huku wakinipa vitisho kuwa nikiendelea kugoma watanipeleka lupango.
Nikaona isiwe kesi maana nazidi kuchelewa futari, nikalipa hiyo elfu 30 na afande boniFace akaniandikia notification na kuniandikia risiti zile za damu ya mzee na kunipa risiti ya malipo na notification.
Naomba niulize hivi ni kweli utaratibu wa kulipa siku nyingine au kulipa kwa mashine za efd upo dar pekee kama alivyodai. Pia ni sahihi kwa askari trafiki kutembea na kitabu cha risiti kile cha kahawia na kukukatia risiti ilihali yeye sio cashier wala mhasibu wa polisi.
Ni sahihi kwa trafiki kumlazimisha dereva alipe faini papohapo bila kujali hali na wakati na kumtisha kuwa asipolipa faini gari inapelekwa kituoni na ukiwa mbishi unaenda lupango.
Mwisho ni sahihi kwa trafiki kupokea hela taslim elfu 30 saa 11 jion kutoka kwa dereVa wakati sheria inamkataza kukaa na hela zaidi ya sh. 500 kama sijakosea na kama sijaridhika na huduma za trafiki husika niende wapi kulipoti malalamiko ya trafiki husika.
Naombeni ushauri wakuu...