Askari Kikosi cha usalama barabarani

Bob Dylan

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
208
223
Watanzania tumefikia mahali tumepata elimu kidogo ambayo inaweza kutuelewesha mambo mbalimbali ikiwemo haki zetu za msingi na sheria nyingine nyingine. Hawa askari wa barabarani hawabadiliki na hawataki kugundua hilo.

Unakamatwa na askari hakueleweshi anachofanya nikukutishia kwa mabavu na ubabe. Jana nilitembelea manyara nkakutana naa hawa jamaa mahali panaitwa nanja kwakweli nimesikitishwa sana na hawa askari wetu namna wanavyolazimishia mambo na wanavyojiskia inferior unapomuelewesha.

Lengo sio kumfundisha kazi lakini kama hajui sheria ukimfundisha inakua ni tabu kabisa. Kuna askari anajiita "mbongo mbabaishaji wa mjini" hakuna mtu anakera kama huyo hajui kitu kichwani lakini ubishi wake haulezeki. Wito kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani nendeni shule na mjifunze kuelewesha raia na kuwaskiliza ubabe sio solution.
 
Watanzania tumefikia mahali tumepata elimu kidogo ambayo inaweza kutuelewesha mambo mbalimbali ikiwemo haki zetu za msingi na sheria nyingine nyingine. Hawa askari wa barabarani hawabadiliki na hawataki kugundua hilo. Unakamatwa na askari hakueleweshi anachofanya nikukutishia kwa mabavu na ubabe. Jana nilitembelea manyara nkakutana naa hawa jamaa mahali panaitwa nanja kwakweli nimesikitishwa sana na hawa askari wetu namna wanavyolazimishia mambo na wanavyojiskia inferior unapomuelewesha. Lengo sio kumfundisha kazi lakini kama hajui sheria ukimfundisha inakua ni tabu kabisa. Kuna askari anajiita "mbongo mbabaishaji wa mjini" hakuna mtu anakera kama huyo hajui kitu kichwani lakini ubishi wake haulezeki. Wito kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani nendeni shule na mjifunze kuelewesha raia na kuwaskiliza ubabe sio solution.
Nadhani ipo haja ya polisi kuajiri wahitimu wa chuo cha usafirishaji (NIT) hao ndio wataalamu wa magari badala ya kuchukua askari walio mahiri katika kupiga kwata. Tunataka maafisa usalama barabarani angalau wawe na degree moja ya sheria usafirishaji au uhandisi (Mechanical engineering).
 
Maaskari wengi hawajui kitu nivilaza, nguo bunduki na ubabe ndio vinawabeba in the name of the law. wanafanyakazi kwa mazoea na si kwa ufanisi. Nahisi wengi wao hawana profession kwasababu always they make noise like empty tins ukitaka kuwafundisha/kuwaelekeza.
 
R.T.O iringa nae ni jipu....huwa anakaa pale mwisho mwa mlima ipogoro..kajaza vitabu vyake vya notification kwenye kigari kidogo....sera yake eti ni kuona vitabu vinaisha vyoge....RTO mtumbo kichwani hakuna kitu....elemisha watu wajue sheria za barabaran sio kuwakatia manotification kama kicha....afu mbona mkidaiwa risti mnabadilika rangi.
Traffic barabaran is another great changamoto kwa kwel.
 
Kilio changu serikali ikataze litrafic kupewa hela na kutoa notification tu na sio risti.....ukidai risti eti uende j3....mbona hela hamuachi had j3....mtu anasafiri mtwara arusha...unamkamata kibiti unamwambia j3 aje kufuata rist......acheni utapeli trafic njaa
 
Back
Top Bottom