DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Gari la askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji visiwani Zanzibar, limepata ajali na kusababisha kifo cha askari mmoja huku wengine wakijeruhiwa.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji visiwani Zanzibar, Kamishna Mzee Abdallah, amesema gari hilo lilikuwa kwenye msafara wake, wakati akikagua maendeleo ya vikosi vya Zimamoto na Uokoaji kisiwani Pemba ambapo walipofika Micheweni, lilipata ajali na kusababisha maafa hayo.
Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni, Rashid Mkasha amesema walipokea jumla ya majeruhi 8 ambao ni askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na mmoja kati yao, alikuwa tayari amefariki dunia wakati akifikishwa hospitalini hapo.
Ameongeza kuwa kati ya majeruhi, watatu hali zao hazikuwa nzuri ambapo walisafirishwa kwa helikopta ya jeshi kwenda kwenye hospitali nyingine kwa matibabu zaidi.