Asili ya Mwafrika,Mzungu na Mtu wa Asia...na siku zetu.

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,314
Katika pita pita katika vitabu vya mzee vya zamani nimefanikiwa kuona kitabu kimoja kikuu kuu,kizee kilichochoka sana na chenye kuonesha kuwa kimekaa kwa miaka mingi sana katika dunia hii.

Ukikiangalia utaona tu kuwa ni cha zaman kwa sababu hata font iliyotumika ni ya zamani sana aina ya font ile ya kwenye type letter. Kimeandikwa "where we are from and where we are" halafu kwa maandishi mwakuba mekundu kimeandikwa "BANNED" Nlishangaa kidogo hiki kitabu kimefika hapa na kinasemekana kuwa ni banned.

kwa wale waliosahau neno ban maana yake ni kupiga marufuku. "banned"kilichopigwa marufuku.
kitabu hiki nlipokisoma kimenifungua kwa kiasi kikubwa hasa kuhusiana na asili ya waafrika,wazungu na waasia na waarabu.
kinasema kuwa hapo mwanzo alikuwepo mama mmoja ambaye yeye hakuumbwa na rangi yeyote ile pamoja na mumewe ambao walikuwa na rangi ya maji yaani colorless. na waliiishi miaka mil 2 iliyopita katika nchi moja yenye milima,mabonde na mito mingi.

wakiwa ni watu wenye miili mikubwa sana na uwezo au nguvu nyingi za kutenda mambo yaani pamoja na akili ambazo walizitumia kwa manufaa ikiwepo kugundua moto,kufua vyuma n.k

waliishi zaidi ya miaka 100,000 wakiwa wao wawili tu. na mwishowe walianza kuhisi kuwa wana ukaribu sana ila wanashindwa kuelewa nini kinawavuta sana kiasi cha kuwa na hali hiyo ya kuvutiwa na kila mmoja wao.
siku zote hawakuwa wakitenda tendo lolote kuhusiana na mapenzi mpaka ilipotokea yule mama aliyekuwa anaitwa Alphaatina alipogundua kuwa kumbe kuna sehemu fulan katika mwili wake ina njia ya kuingiza kitu.

hivyo akamwambia mumewe Alphaabrina kuwa kuna sehemu ameiona anashindwa kuielewa ni ya nini. mumewe naye akashika ile sehemu kama alivyooneshwa na mke. mara akaona uume wake ukisimama. na hatimaye wakaamua kujaribi kufanya mapenzi na yakaanzia hapo. nimejaribu tu kuikata.

baadaye walianza kuwa wanaenjoy sana na mwishowe yule mama alishika mimba akaja akazaa mtoto pamoja wakashangaa sana na kumwita mtoto talifaat. taalifat alitoka akiwa na rangi nyeusi. walimpenda yule mtoto wakiona sasa nao wamepata mwenzi wao. mama akapata mimba tena akamzaa mtoto mwingine.

huyu aliitwa Araahitlaf alikuwa na rangi nyeupe nyeupe na pua kubwa iliyolala kwa mbele kidogo. na baadaye tena waka mzaa Zangakli aliyekuwa mweupe zaidi na mwenye pua ya kuchongoka.

waliishi kwa muda mrefu kabla ya kupata tena watoto wawili wa kike. araahitlaf alitembea na dada yake na talifat naye pia akaamua kulala na dada yake huyo huyo. araahitlaf alipoona dada yake ametembea na kaka yake alipatwa na hasira sana na kutaka kumuaa kaka yake. ugomvi ulisuluhishwa na wazazi na hatimaye kwaamua yule dada achague anataka kuishi na nani. yule dada akamchagua araahitlaf.

talifat alisikitika sna maana naye alikuwa ameshaonja ladha ya mapenzi.hatimaye akawa ni mtu mwenye majonzi na kulalamika kila mara. yule mtoto wa mwisho yeye alikuwa ni mtu ambaye yupo busy sana muda mwingi alikuwa akipanda kwenye miti akienda porini na alionekana ni mtundu sana. mtoto wa kwanza yeye alipenda kukaa miguuni kwa wazazi hasa mama yake.

wkati wa pili yeye alikuwa na mke wake tu na kwa kuwa sasa hakumwamini hakutaka hata kuwa mbali naye.
baadaye wale wazazi wakamzaa tena mtoto wa kike mwingne huyu wa kike mwingine akawa amekua na akaanza uhusiano na mtoto wa kwanza. na ikawa sasa huyu wa mwisho yeye hana mtu . yeye akawa sasa anaenda porini anawinda analeta nyama anawaambia wale kaka zake atakayempa mke wake alale naye ndiye atakayepata nyama.ikawa wanampa hivyo ili alale na wake zao. huko wakazaliwa watoto wawili kutoka kwa dada hao Tinanching na Lidvanchindiah...

yule kijana wa mwisho akawa anawatawala wale kaka zake. kwa kuwa alikuwa na akili na ubinifu mwingi. yule kwa kwanza alibobea sana kwenye mapenzi na kutulia miguuni kwa wazaz wake huku akilalamikia ngozi yake kuwa ni kikwazo hasa baada ya kuwa mkewe wadogo zake waliweza kutembea naye. yule wa kati kati alionekana kutokuwa na huruma kwa wenzie akiwafanyia fitna na hujuma mbalimbali ili aogopwe kwa sababu kimwli alikuwa na udhaifu.

wa mwisho aliendelea kuchapa kazi akaoa akaeneka kuishi kwa amani.............nitaendelea kuielezea historia ya asili ya wazungu,waafrika,waarabu/asia.
 
Hichi = hiki. Well, ninacho nmekitunza vizuri kwa ajili ya kujisomea tu kujua myth mbalimbali kuhusiana na uumbaji.
Ahsante. Natamani siku moja nikione hiyo story niliwahi sikia kuhusu hao watu wasiokua na rangi ila aliyekua ananisimulia alisema Mungu ndio aliwaumba wakiwa hawana rangi
 
Mkuu GuDume, mimi ni miongoni mwa wale wanaovutiwa sana na mtindo wa uwasirishaji wako wa mada. Ndiyo maana nilitamani sana uniharirie kitabu changu ninachoendelea kukiandika. Ingawa sina hakika pia kama una muda kama huo.
 
Back
Top Bottom