Asanteni sana Wapendwa

Asanteni sana Wapendwa

Strawberry

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
274
Reaction score
108
Habari wana Jamii Forum.
jamani Jamani hata sijui nianzie wapi jamani.Ila nawashukuruni kwa sala zenu na maombi yenu.
Tumemaliza msiba wa Mme wangu mpendwa salama.Namwombea Mungu ampe pumziko la milele.

Kweli nashukuruni wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine adi kumafanikisha mkumpuzisha salama Marehemu Mme wangu.Japo ni ngumu sana kwa upande wangu kuamini kama kweli nimeondokewa na Mme wangu ila sina budi kumshukuru Mungu baba.Kweli ntalia siku zote za maisha yangu maana nimeachwa bado umri wangu mdogo na bado nilikuwa nategemea yeye aniongoze katika maisha haya.

Lakini sina budi ya kufunga mkanda na kupigana kiume adi nikuze watoto wangu tuliobahatika kupata na Mme wangu.

Nawasihi wanandoa jamani pendaneni na heshimianeni kila mmoja aone umuhimu wa mwenzie.Hata kama ni chongo hana mvuto jamani siku akikutoka ni majuto tu jamani.

Asanteni sana
 
Pole kwa maswaibu na mtihani uliokupata...Mungu akurejeshee faraja.
 
Pole mamii,Mungu na akupatie faraja unayostahili
 
Pole sana mumie..Mungu ni mwema atakusimamia imara na Watoto wako watakua vizuri kabisa..Ubarikiwe.
 
Pole my dia.......uchungu wa kuondokewa mtu umpendaye ni mkubwa sana......

mungu aendelee kukutia nguvu
 
pole sana,amini Mungu atakuwezesha kuwalea watoto wako na kuwatunzeni nyote kupitia hekima na busara zako,kaza moyo bado una safari ndefu sana....
 
Pole sana mpendwa Mungu akupe nguvu na maarifa ya kulea watoto
 
Pole sana jamani...........Mungu akupe faraja na ujasiri kukabiliana na changamoto zitokanazo! Na usimame imara!
 
Habari wana Jamii Forum.
jamani Jamani hata sijui nianzie wapi jamani.Ila nawashukuruni kwa sala zenu na maombi yenu.
Tumemaliza msiba wa Mme wangu mpendwa salama.Namwombea Mungu ampe pumziko la milele.

Kweli nashukuruni wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine adi kumafanikisha mkumpuzisha salama Marehemu Mme wangu.Japo ni ngumu sana kwa upande wangu kuamini kama kweli nimeondokewa na Mme wangu ila sina budi kumshukuru Mungu baba.Kweli ntalia siku zote za maisha yangu maana nimeachwa bado umri wangu mdogo na bado nilikuwa nategemea yeye aniongoze katika maisha haya.

Lakini sina budi ya kufunga mkanda na kupigana kiume adi nikuze watoto wangu tuliobahatika kupata na Mme wangu.

Nawasihi wanandoa jamani pendaneni na heshimianeni kila mmoja aone umuhimu wa mwenzie.Hata kama ni chongo hana mvuto jamani siku akikutoka ni majuto tu jamani.

Asanteni sana

Pole sana dada, Mwenyezi Mungu akupe nafuu ma nguvu katika kpindi hiki kigumu
 
Back
Top Bottom