Asante TBC taifa kwa kuipendezesha weekend yangu kupitia kipindi hichi cha nyimbo za injili.

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,108
35,928
Baada ya pilikapilika za mwezi mzima mikoa mbalimbali nchini katika harakati za kutafuta pesa ili maisha yasonge hapa Tz.

Mimi sio mtu wa mitungi ila nagusa gusa kidogo nikiwa na wapambanaji wenzangu ile ku socialize na kupeana michongo ya utafutaji pesa.

Hivyo leo wikiendi nimepata kupumzika na familia...katika harakati za kubadili channel kutoka kwenye king'amuzi cha dstv.

Nikakutana na kipindi cha nyimbo za injili kutoka kwa ndugu zetu wa kiimani wasabato...hakika hawa watu wanajua kuimba sana..wanapangilia sauti vilivyo pamoja na ala za muziki.

Pia uvaaji wao ni wakupendeza na natural hakuna ile miwingi mi heleni mi mekapu wako katika uhalisia,hongera kwa kanisa kusimamia misingi hiyo...kongole kwao.

Hivyo kufanya moyo na mwili uweze kubarikiwa na kupata tulizo la kiroho kupitia uimbaji wao..wabarikiwe sana hawa waimbaji wa kisabato.

Tbc kwa hili nawapa kongole..ikiwezekana waongezeeni muda lisaa limoja halitoshi.

Mungu awabariki sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom