ASANTE SANA ALLAH KWA 2024

ASANTE SANA ALLAH KWA 2024

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
227
Reaction score
246
.

Anaandika Mo Mlimwengu.

Huyu huyu Mwenyezimungu muumbaji wa ardhi na mbingu. Huyu huyu ambaye ni Mfalme, mtakatifu, mwenye kutupa salama na kutupa amani. Huyu huyu anayeendesha mwenyewe mambo yake pasipo na msaada wa kiumbe yeyote.Huyu huyu mwenye nguvu na anayefanya jambo analolitaka. Acheni bwana huyu ndiye muumbaji, muundaji, msanifu mkubwa na mwenye kila majina mazuri kabisa . Na kila kilichoko katika mbingu na ardhi kinamtakasa na ndio huyu huyu mshindi na mwenye hekima zaidi.

Mlimwengu mimi si chochote si lolote ila huyu huyu Mwenyezimungu ndio alinipa kibali cha kuzunguka na hii dunia kuhakikisha napita kwenye barabara nzuri na barabara mbaya. Akanipitisha kwenye mitihani mikubwa na midogo. Lakini huyuhuyu akanipa kibali cha kuendelea kusimama kila sehemu ambayo kwa macho ya kawaida huenda wangesema nisingevuka. Wakati dunia inakamilisha utaratibu wake wa kulizunguka jua na kujizungusha kwenye mhimili wake. Huyu huyu Allah akaendelea kunilinda mimi kiumbe wake dhaifu lakini bado kaendelea kunilinda na kunipa afya iliyopo. Ukubwa wake sina budi kuulinganisha na chochote. What a miracle? Acha tu Mungu ni mkubwa mno na hana mfanowe.

Kuna waliojivisha ngozi ya binadamu kumbe siyo wakajipa vyeo vyote. Wakawa mahakimu wao wakasahau hakimu yupo ni huyo huyo ambaye tunamcha usiku na mchana. Wakageuza vinywa vyao kunenea wenzao mabaya. Haohao wakajifanya ni watabiri kwa kujua maisha ya wenzao. Lakini huyu huyu Mwenyezimungu akaendelea kutukumbusha kwamba yeye ndio wa pekee na ndio mwenye kuendesha yote na ndio mwenye kustahili kuabudiwa peke yake. Kuna watu walijipa vyeo vya urafiki na ndugu zetu huku wakitegeshea tufanye kosa moja wapate sababu ya kutukataa. Lakini huyu huyu tunayemuabudu kaendelea kusimama na sisi na kwa uwezo wake ameendelea kutukumbusha kujua zipi mbivu na zipi mbichi.

Asante sana Mungu kwa 2024.Kuna wengi ambao tulianza nao safari ya mwaka 2024 lakini ni wewe Mwenyezimungu uliyeamua mlimwengu mimi niendelee kushuhudia rehema zako hadi sasa. Kwenye safari hii tumepoteza baba zetu, mama zetu, watoto wetu, majirani wetu na ndugu na jamaa wa karibu. Lakini wewe ndio umeamua kutupa kibali cha kuendelea kuishi. Mimi ni nani nisikusifu? Mimi ni nani nisikuabudu? Mimi ni nani nisiendelee kukushukuru na kutumai kwamba yajayo yanafurahisha.

Kasinge muno Rugaba.

#mlimwengumimi
#kwaheri2024
#karubu2025
#Allahakbar
 
Back
Top Bottom