chambi1509
Member
- Mar 29, 2018
- 95
- 42
Imekuwa ni muda sasa tangu sheria mpya inayohusu kulipa mpaka mwanachama afikishe umri wa miaka 55-60 kulipwa mafao yake pasipo kuzingatia sababu za kuacha au kupoteza ajira ya MTU husika!
Lakini sasa Nssf kupitia tawi la Tarime nawapongeza kwa kuamua kuwalipa waliokuwa wanachama wenu japo wameteseka,wamenyanyasika na kudumaa ingawa pesa yao mlikuwa mmeing'ang'ania kwa zaidi ya miezi nane (8). Huku wale wanachama waliokuwa Ppf wakichukua pesa zao mapema tu (ndani ya wiki tatu Mara baada ya kuachishwa kazi na mgodi wa acacia-north Mara)
Kwa sasa kuanzia Jana mmeanza kutoa pesa hiyo, pasipo na huruma baadhi ya wafanyakazi wenu (Nssf employees) mnataka kupewa rushwa ili muitoe pesa hiyo kwa kisingizio cha kuwahisha, SASA MNAWAHISHA NINI WAKATI PESA YENYEWE IMECHELEWA KUTOKA?
KWANINI MNAKOSA HURUMA YA KUWAONEA HURUMA HAWA WATU, UKIANGALIA WAMESHAKOSA AJIRA, NYIE BADO MPO KWENYE AJIRA NA HILI JASHO LAO MNATAKA MPATE MGAO???
Huu sio uungwana hata kidgo! Jitathimini na muwe na HURUMA ya mungu!
Ni hayo tu!
Sent using Jamii Forums mobile app