Asante Lionel Messi, kila la heri fundi wa mpira ambae mimi nimekushuhudia

Jerry Rebiam

JF-Expert Member
May 22, 2016
402
357
Mimi Jerry Rebiam Medson Kyando ni mshabiki mkubwa na lia lia wa Barcelona Fc na Simba kwa Hapa Tanzania, kwa kipind cha hii miaka mitatu sikufurahishwa na matokeo ya Barcelona kwa upande wa champions league kuanzia matokeo ya 3 kwa 0 dhidi ya As Roma ...4 kwa 0 kutoka kwa Liverpool na hasa magoli 8 kwa 2 kutoka kwa Bayern Munich.

Nilichogundua matokeo haya yalisababishwa na hasa kuwa na team ya kawaida iliojengwa kumzunguka mchezaji mmoja yaani Lionel Messi, niliumia sana matokeo dhidi ya Liverpool kwani kipindi cha kwanza our Jord Alba alikia na chance ya kuumaliza mchezo kwenye kipind cha kwanza pale Anfield ila alifanya kitu kilichoudhi sana kwa kuurudisha mpira kwa Messi wakati yeye alikua na 95 za kufunga na kwa bahati mbaya Messi alipoteza ile nafasi. Team yangu haijawah kukubali kua Vidal, Busquet, Rakitic, Pique na Alba kuwa uwezo wao umeisha na tulipaswa kuunda team ya kiushindani. Asante Roma; Liverpool na PSG kwa kutupa alarm ya kuwa Barcelona uwezo wetu kiushindani ulikua umeisha pamoja na kiburi chetu, asante Bayern Munich kwa kutuambia kuwa tunahitaji kujiangalia upya.

Kwa upekee asante Lionel Messi kwa kukataa kuendelea na club yetu kwani unatupa nafasi ya kuitengeneza upya team yetu bila kukuzunguka wewe, huu ni upendo mkubwa sana. Mimi Jerry Rebiam nitaheshimu na kukumbuka uwezo wako uwanjani na nitakushabikia hata ukihamia Yanga, natamani usiangalie nyuma na uzidi kusimamia msimamo wako.

Kila la heri fundi wa mpira ambae Mimi nimekushuhudia # Lionel Messi
 
Et hata
Hata hakiamia yangu
 
Anastaafu au anahama timu?
Kama anasikia ushauri, astaafu. Hana uwezo wa kucheza mpira nje ya Barcelona na pengine niseme hana uwezo wa kucheza mpira wa kipindi hiki cha falsafa ya kukusanya wachezaji wazuri toka sehemu mbalimbali na kuunganishwa kwenye timu moja, mpira wake ni wa kucheza na wale aliozoeana naye kwa mahitaji yake. Mathalani angekuwa anacheza EPL ya kipindi kile ambapo wapishi wengi walisifika kwa kunyoosha goti, nani angekuwa anampikia n kumuoshea vyombo kama walivyofanya wakina Xavi, Iniesta n.k?
 
ManCity
 
Uwezo haujifichi na uhakika ata akienda epl Bado atakichafua
Kama EPl ninayoifahamu haijabadilika, basi niko kusubiri huo uchafu. Kama CR7 alienda Laliga na kuvunja rekodi ya mfungaji bora kabla Messi hajaifikia. Basi angalau afikie rekodi moja tu hata ya Thierry Henry kwa msimu wa kwanza kwakuwa ndio msimu wa mwisho yeye kucheza soka lenye harufu la uwezo mkubwa
 
Ataweka Record yake we subir utaona
 
Tusubir tuone
 
Epl itakuwa ngumu sana kw Babu Messi, hataimudu na asitegemee ataendlea kuwa bora kwa kwenda Epl
 
Mimi ni shabiki mkubwa wa barca na messi .. Barcelona imeshuka Sana kiuwezo kiasi kwamba Inamshushia hadhi messi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…