Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 959
Usichokijua ni kwamba 2015 CCM iliamua kuweka wagombea wawili!Declaration of interests: Mimi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa, wala sina utaalamu mkubwa wa mbinu za kisiasa. Mimi ni mtanzania huru na mwenye maoni huru.
Licha ya kazi iliyofanywa na sekretarieti ya CCM katika kulikata jina la Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha wagombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watanzania wengi waliingia mkenge wa kumshabikia fisadi Lowasa baada ya kuhamia ukawa.
Baada ya tuhuma zake nyingi za ufisadi wa mabilioni ya shilingi, mpaka chama chake kumtupa, tuliona jinsi ndugu Lowasa alivyohangaika kwa uchu wa kutaka urais hata ikabidi kutimkia ukawa. Kwa uzee ule na uchovu aliokuwa nao huku akitetema hovyo, hata mimi nilishawishika kuamini huenda angetutoka punde.
Sifahamu kama ni mbinu za kiintelijensia na usalama wa taifa, au ni figisu, hatimaye Jaji lubuva akamfutilia mbali ndugu Lowasa kupitia sanduku la kura huku wafuasi wake wakiachwa macho kodo wakihuzunika kama makinda ya njiwa.
Wakati tukiwa tunastaajabu kwa butwaa, Magufuli akachanja mbuga kwa kasi mpaka ikulu na kutwaa mamlaka. Lakini kwa uchungu, ukawa wakabaki na fisadi lao huku wasijue walitupe wapi.
Hatimaye, lowassa katimkia CCM, na anasema amerudi nyumbani! Tunajifunza nini? Je, mwanasiasa ni mtu wa kuaminika?
Mtu anayeweza kuwasaliti watu million sita waliokesha kumpigia kura, kumdekia barabara, kumsapoti na kumshangilia, mpaka wengine wakavunjwa miguu na polisi?? Huyu mtu anafaa kuongoza nchi? Ana ajenda gani? Ana aminika vipi?
Asante Lubuva kwa kumfyekelea mbali huyu masai uchwara mwaka 2015. Haukukosea . Viva Lubuva.
Shkamoo CCM.Usichokijua ni kwamba 2015 CCM iliamua kuweka wagombea wawili!
Doohh![emoji23][emoji23][emoji23]Mabadiliko-lowasa
Lowasa-mabadiliko
UKIWA hatutasahau siku Ile tumekwenda kuzungushwa mikono pale jangwani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni sawa na ile hadithi ya samson alipomuua simba, baadae nyuki wakatengeneza asali kwenye mzoga wa simba. Yes, huenda ni kweli Magufuli alishinda kupitia mfumo mbovu.Japo una hoja lakini kutendo cha kushabikia mfumo mbovu wa uchaguzi wa Jaji Lubuva, sikuungi mkono !!. Hata ikiwaje hatutakiwi kuwa na tume iliyo na matokeo kabla ya kura kupigwa !!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sina chuki na Lowasa wala mwanasiasa yeyote, na kiufupi sishangilii kuwa na tume mbovu ya uchaguzi.kama chuki yako dhidi ya Lowasa inakufanya umshukuru Lubuva kwa kukiuka katiba na kuwanyang'anya watanzania haki ya kuchagua kiongozi wao basi kichwani hauko sawa!! kama unamshukuru Lubuva kwa kusoma motokeo halisi aliyopaswa kuyasoma kwa mujibu wa sheria sielewi unamshukuru kwa lipi??
Kawadhihaki sana wale ndugu zangu waliohangaika kumpa support ya hali na mali. Huyu morani ni kimeo, hafai hata kuongoza familia. Ndio maana kumbe akina Nape walisimama kidete kumshughulikia.EL ni haki yake.Anazo sababu binafsi, Ila kwa hili kawadhulumu na kuwadhihaki wafuasi wake.
Sent using Jamii Forums mobile app
DECLARATION OF INTEREST: Mimi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa, wala sina utaalamu mkubwa wa mbinu za kisiasa. Mimi ni mtanzania huru na mwenye maoni huru.
Licha ya kazi iliyofanywa na sekretarieti ya CCM katika kulikata jina la Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha wagombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watanzania wengi waliingia mkenge wa kumshabikia fisadi Lowasa baada ya kuhamia UKAWA.
Baada ya tuhuma zake nyingi za ufisadi wa mabilioni ya shilingi, mpaka chama chake kumtupa, tuliona jinsi ndugu Lowasa alivyohangaika kwa uchu wa kutaka urais hata ikabidi kutimkia UKAWA.
Kwa uzee ule na uchovu aliokuwa nao huku akitetema hovyo, hata mimi nilishawishika kuamini huenda angetutoka punde.
Sifahamu kama ni mbinu za kiintelijensia na usalama wa taifa, au ni figisu, hatimaye Jaji lubuva akamfutilia mbali ndugu Lowasa kupitia sanduku la kura huku wafuasi wake wakiachwa macho kodo wakihuzunika kama makinda ya njiwa.
Wakati tukiwa tunastaajabu kwa butwaa, Magufuli akachanja mbuga kwa kasi mpaka ikulu na kutwaa mamlaka. Lakini kwa uchungu, UKAWA wakabaki na fisadi lao huku wasijue walitupe wapi.
Hatimaye, leo hii Lowasa katimkia CCM, na anasema amerudi nyumbani! Tunajifunza nini? Je, mwanasiasa ni mtu wa kuaminika?
Mtu anayeweza kuwasaliti watu million sita waliokesha kumpigia kura, kumdekia barabara, kumsapoti na kumshangilia, mpaka wengine wakavunjwa miguu na polisi?? Huyu mtu anafaa kuongoza nchi? Ana ajenda gani? Ana aminika vipi?
Asante Lubuva kwa kumfyekelea mbali huyu masai uchwara mwaka 2015. Haukukosea . Viva Lubuva.
Shkamoo CCM.
Watatu.....usimsahau mamayetu aliyekua anazunguka na benz la pinkiUsichokijua ni kwamba 2015 CCM iliamua kuweka wagombea wawili!
Wafuasi wake anarudi nao CCM!EL ni haki yake.Anazo sababu binafsi, Ila kwa hili kawadhulumu na kuwadhihaki wafuasi wake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana kabisa. Mimi sina uhusiano wowote na CCM wala CHADEMA.Sio mshabiki wa chama chochote cha siasa wala huna utaalamu wa mambo ya siasa!! Usione aibu kusema uko ccm.
Sina chuki na Lowasa wala mwanasiasa yeyote, na kiufupi sishangilii kuwa na tume mbovu ya uchaguzi.
Sifahamu kama matokeo yalikuwa halali ama yalichakachuliwa, lakini naamini Lubuva alifanya vyema kumtangaza mshindi Magufuli.
Hata hivyo, ingetufaa nini kuwa na tume nzuri ya uchaguzi halafu akachaguliwa huyu morani asiyeaminika?