Arusha wavuka Malengo ya Ukusanyaji

kwedikwazu

Member
Dec 17, 2016
18
15
Ufinyu wa Mapato ya ndani ni dondandugu kwa Halmashauri nyingi hapa Tanzania. Kwa miaka na miaka kumekuwa na kilio cha Halmashauri kushindwa kukusanya mapato na kutegemea fadhila za mapato Serikali kuu jambo linaloweka vizingiti kwa maendeleo katika maeneo yao.

Hali ni tofauti huko Arusha ambapo Mkurugenzi wa Jiji la hilo, Athumani Kihamia (anayeonekana pichani ) akishirikiana na watendaji wengine wa jiji hilo wanaonyesha mfano wa kipekee. Ubunifu, uadilifu na uchapakazi wa watendaji wa Arusha unamiminisha mamilioni katika mifuko wa Jiji lao.

Katika mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Jiji la Arusha ilipanga kukusanya Tsh Bil 12,299,585,000 kama mapato ya ndani. Kwa wengine ilionekana miujiza kwamba fedha hizo zisingeweza kukusanywa kwa mwaka huo ( yaani kati ya Julai 1 2016 hadi Juni 30 2017 )

Arusha imetekeleza, hadi Mei 22 2017, Jiji hilo limefanikiwa kukusanya Bil. 12,324,278,804. Hii ina maana kwamba Jiji limevuka malengo huku mwezi mmoja ukisalia kabla ya kukamilika kwa mwaka wa fedha ( Juni 30 ) na hivyo wanatajia kuongeza zaidi ya bilioni 1 kwa kuzingatia kwamba wastani wao ukusanyaji wa mapato ni shilingi bilioni 1.4 kwa mwezi.

Licha ya kwamba Serikali kuu inaendelea kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo ya Jiji la Arusha,Halmashauri ya Jiji hilo inastahili kila aina ya sifa na kuwa mfano wa kuigwa kwa Halmashauri nyingine.
8d34b1a9a22b308ed324e5fe2a15c81d.jpg
 
Jimbo likiwa chini ya chama pinzani, masuala ya maendeleo, ukusanyaji kodi na matumizi huwa ni mfano wa kuigwa na kupongezwa na serikali kuu, nahakika tuzo ya ngao ya halmashauri zinazofanya vizuri lazima itakwenda kwa majimbo yaliyo chini ya umoja wa UKAWA.
 
Huyo mkurugenz ni jembe na ni namba moja kwa wakurugenz wote niliowah kuongozwa nao tangu nianze kaz
 
Hizo pesa zibadilishwe haraka kuwa maendeleo. Ukusanyaji peke yake hautakuwa na maana kama mtoa kodi hanufaiki.
 
Back
Top Bottom