VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro hapa Arusha vimeshafurika wananchi wa Arusha. Wapo hapa kumsubiri Mbunge wao wa Arusha Mjini na Viongozi wenzake wengine ambao watafanya mkutano wao wa hadhara wa kimaendeleo kuanzia saa tisa alasiri ya leo.
Kila mmoja aliyepo hapa na anayetazamiwa kuja hapa Ngarenaro ana lengo lake. Wapo wanaohitaji kumuona tu Mbunge wao Lema ambaye hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa miezi minne. Wapo wanaomngoja aseme nao neno hata moja. Wapo wanaosubiri aseme mipango ya kimaendeleo na jinsi anavyoitekeleza.
Ukipendwa na wananachi waliokuchagua unapata nguvu. Lema ni mfano wa viongozi wa kuchaguliwa anayekubalika katika uwanja wake wa nyumbani: Arusha Mjini. Lema anaonwa kama kiongozi wao; mtu wao wa karibu; mtoto wao; kaka yao; baba yao; msemaji na mtendaji wao; kioo chao na kadhalika. Kama mwanaCCM, nausema ukweli huu hata kama ni mchungu.
Lema anatajwa kama Mbunge aliyeing'arisha Arusha kwakuwa wanaArusha wanafanya mambo yao kwa uhuru kwakuwa 'wana Lema'. Anapendwa zaidi ya kupondwa na wanaArusha kwa misimamo yake; hoja zake; na uthubutu wake. Lema ni nguzo,si tu ya CHADEMA hapa Arusha, bali ya wanaArusha popote walipo.
I personally admire him and his actions and struggles. WanaArusha wapo hapa Ngarenaro tangu asubuhi wakisubiri mkutano. Ni kama wanaSimba/wanaYanga wanapojazana Taifa kusubiria mtanange wa watani hao wa jadi.
Mwafaaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)