ARUSHA: Mwanajeshi wa JWTZ achomwa kisu na kibaka na kufa akiokoa simu iliyoibwa

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Taarifa kutoka Arusha inasema Mwanajeshi mmoja wa JWTZ amechomwa kisu na vibaka walioiba simu alipoingilia kati kuiokoa hiyo simu iliyoibiwa huko Matejoo Arusha na hao hao vibaka.

Alikuwa alijitolea RAIA mwema aliyeporwa hiyo simu na vibaka na yeye kushuhudia ndipo alipojitosa kuokoa jahazi na bahati mbaya vibaka nao wakamuwahi kumjeruhi na visu.

Tuko la kusikitisha sana kwa wapiganaji wetu vs wanainchi

Update:
ARUSHA: Askari wa JWTZ, MT 94293, Tekeli Israel (29), ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na watu wanaodaiwa kuwa ni vibaka.
 
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.

Hao vibaka watakamatwa tu na huenda ikawa mwisho wa wao kuwepo mahala hapo. Kichapo kitakachotolewa hapo, Mungu ndiye anajua.
Kuna nn kwenye nchi hetu mbona mauji hasa askar yamezid? Dah tumuombe mungu atuepushe na tufan hii.
 
Back
Top Bottom