ARUSHA: Mkuu wa Mkoa atengua ada ya vitambulisho kwa watumishi wa umma

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Serikali imefuta ada ya sh 5000 iliokuwa wanakatwa watumishi wa umma kwaajili ya kutengeneza vitambulisho vyao vya kazi. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi wa umma, Watumishi Mkoani Arusha wamekua wakikatwa sh 5000 na maafisa utumishi kwaajili ya kuandaa na kuwatengenezea vitambulisho vya kazi watumishi wa umma.

Chanzo: ITV
 
Hio halmashauri inaongozwa na cdm badala ya kua mfano kwa wengine, lakini inaongoza kuanyonya walimu ujinga wa,
 
Vitambulisho vinamhusu MKurungezi, DED kateuliwa na nani?
Katika Halmashauri Hakuna kinachofanyika bila idhini ya baraza la madiwani, hivyo chadema kama wanaongoza hiyo Halmashauri watakuwa wanahusika
 
Siyo kweli mkuu hata kidogo nakataa, nimefanyakazi halmashauri kwa kujitolea kwa mwaka mzima.
 
Hio halmashauri inaongozwa na cdm badala ya kua mfano kwa wengine, lakini inaongoza kuanyonya walimu ujinga wa,
Ashukuriwe Mungu, kwa kufanikisha uzaliwe, lasivyo njaa inayotusumbua ingelikuwa mara tatu ya hii.
 
Serikali imefuta ada ya sh 5000 iliokuwa wanakatwa watumishi wa umma kwaajili ya kutengeneza vitambulisho vyao vya kazi. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi wa umma, Watumishi Mkoani Arusha wamekua wakikatwa sh 5000 na maafisa utumishi kwaajili ya kuandaa na kuwatengenezea vitambulisho vya kazi watumishi wa umma.

Chanzo: ITV
Kwa kukurekebisha sema mkuu wa mkoa arusha katengua ada ya vitambulisho mkoani humo. Lazima ujue kutofautisha tamko la mkuu wa mkoa katika mkoa wake na tamko la serikali kitaifa, angetangaza waziri mkuu au mawaziri wa wizara husika au rais hapo sawa ingekuwa tamko la serikali kwa maana kwamba kitaifa ,,ila hapo ni mkoan arusha pekee maana mkuu wa mkoa hana mamlaka kutoa tamko kitaifa.
 
Katika Halmashauri Hakuna kinachofanyika bila idhini ya baraza la madiwani, hivyo chadema kama wanaongoza hiyo Halmashauri watakuwa wanahusika
Si kweli mkuu unapotosha na unajianika kiwango chako cha elimu kuwa hakija kidhi kujadili maswala haya ni lazima mfike mahali muwe mnakubali kuwa kuna mambo yapo juu ya uwezo wenu wa mawazo na fikra sio kila kitu ni siasa tu kuna utaalamu unahitajika kujadili baadhi ya mambo ,

Hebu kasome majukumu ya madiwani katika halmashauri kwa mujibu wa sheria na pia pitia taratibu za utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria ,halafu urudi tena mbio mbio ,maswala ya utumishi yanamuhusu MKURUGENZI,DAS/RAS,AFISA UTUMISHI na WAKUU WA IDARA kwa ngazi ya haolmashauri madiwani hawahusiki hapo mkuu usikalili. Ukitaka kujua uhusika na mipaka yao tafuta kitabu cha majukumu yao ujue yanaishia wapi kwa mtumishi wa uuma
 
Kama hawahusiki mbona wanafanya vikao vya kuwajadili watumishi mbalimbali na kutoa mapendekezo ya kusimamishwa kazi au kufukuzwa?
 
Soma vizuri bandiko langu ndio maana nimekwambia kasome ujue mipaka yao ina anzia wapi na inaishia wapi kwa mtumishi wa umma na lengo la kukuandikia hivyo nilijua kuwa lazima utakuja na hoja hiyo maana hujui mipaka ya diwani kwa mtumishi wa umma ,swala la vitambulisho vya watumishi halipo chini ya mamlaka ya diwani na halimuhusu diwani tambua hilo kwanza, na ujue kuwa hayo mapendekezo akiyatoa diwani anapeleka kwa nani? Hadi hapo tu panatosha kukufahamisha mamlaka ya diwani inaishia wapi kwa mtumishi umma.
 
Mkurugenzi ni wa chadema??? Tumia akili na uwe unaongea mambo unayo yajua sio siasa kila mahali maswala ya utumishi hayahusiani na hayo uyasemayo na ndio maana katajwa afisa utumishi na sio diwani. Shame
Mkurugenzi anatekeleza mipango iliopangwa, na madiwani acheni kujitoa fahamu
 
Serikali imefuta ada ya sh 5000 iliokuwa wanakatwa watumishi wa umma kwaajili ya kutengeneza vitambulisho vyao vya kazi. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi wa umma, Watumishi Mkoani Arusha wamekua wakikatwa sh 5000 na maafisa utumishi kwaajili ya kuandaa na kuwatengenezea vitambulisho vya kazi watumishi wa umma.

Chanzo: ITV
RC ameongea kwa upande wa Mkoa wa Arusha pekee siyo nchi nzima, sikweli serikali imetengua ada ya vitambulisho. Kauli ya RC ni ndani ya mkoa husika siyo nchi nzima mkuu, kauli kama hiyo ingetolewa na Waziri hapo ingekuwa nchi nzima.
 
Si kweli mkuu unapotosha na unajianika kiwango chako cha elimu kuwa hakija kidhi kujadili maswala haya ni lazima mfike mahali muwe mnakubali kuwa kuna mambo yapo juu ya uwezo wenu wa mawazo na fikra sio kila kitu ni siasa tu kuna utaalamu unahitajika kujadili baadhi ya mambo ,

Hebu kasome majukumu ya madiwani katika halmashauri kwa mujibu wa sheria na pia pitia taratibu za utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria ,halafu urudi tena mbio mbio ,maswala ya utumishi yanamuhusu MKURUGENZI,DAS/RAS,AFISA UTUMISHI na WAKUU WA IDARA kwa ngazi ya haolmashauri madiwani hawahusiki hapo mkuu usikalili. Ukitaka kujua uhusika na mipaka yao tafuta kitabu cha majukumu yao ujue yanaishia wapi kwa mtumishi wa uuma
Mkubwa si ueleze unachokijua au weka link kuliko kusema kasome kitabu au sheria fulani kitabu gani wakasome wapi?
 
Back
Top Bottom