ARUSHA: Kituo Cha Radio Five kufilisiwa, chadaiwa milioni 31.9... wafanyakazi waiomba mahakama kuuza Jengo na vifaa vya kurushia matangazo

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mahakama kuu masijala Ndogo ya kazi Kanda ya Arusha imeahirisha kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tan communication inayomilikiwa na waziri Mstaafu Edward Lowasa pamoja na kituo cha Radio Five na waliokuwa wafanyakazi Saba wa radio five wanaodai zaidi ya sh, milioni 31.9 baada ya kuachishwa kazi kinyume na utaratibu.

Wafanyakazi hao wakiongozwa na Geoffrey Steven walifungua kesi hiyo namba 151 ya mwaka 2020 baada kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama yausuluhishi (CMA) iliyompa ushindi mdaiwa.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Naibu Msajiri wa mahakama ,Ruth Masamu ilikuja katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa ,ambapo upande wa walalamikaji wakiongozwa na wakili Heri Makando walikuja kuiomba mahakama hiyo itoe idhini ya kukamatwa Mali za mdaiwa ambaye ni Tan Communication na kupigwa mnada ili kufidia malipo ya wafanyakazi hao.

Hata hivyo wakili wa upande wa mdaiwa,Andrew Maganga ameiambia mahakama hiyo kwamba amewasilisha notisi mahakama kuu ya rufaa kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Johannes Masara , June 16 ,2020 iliyowapa ushindi wadaiwa.

Naibu msajiri wa mahakama hiyo ,Ruth Masamu baada ya kupokea maombi hayo yaliyoambatana na notisi hiyo aliahirisha shauri hilo hadi Machi 16 mwaka huu.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Geoffrey Steven alisema kimsingi wamepokea kusudio la rufaa kwa upande wa wadaiwa na wanachosubiri no tarehe ya kusikiliza kwa rufaa hiyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa leo walikuja mahakani hapo kwa ajili ya kuiomba mahakama hiyo iweze kutoa idhini ya kukamatwa kwa Mali za mdaiwa ambazo ni Jengo la kituo Cha Radio five, lililopo Njiro ploti namba 153 na 154 block J , Jenereta,vifaa vya studio na vifaa vya kurushia matangazo.

Wadai wengine wa shauri hilo ni Monica Nangu , Gloria Kaaya ,Godluck Kisanga , Godfrey Thomas ,Akidai kilango na Josephzat Nyamkinda.


 
Mkuu achana naye sisi TUMEMPUUZA !.
 
Hao wafanyakazi wnyewe hata kazi waliyokuwa wanaifanya hakua kama si kuuza sura na kufanya kazi za nje ya ofisi kwa kutumia ofisi kwa muda mrefu,na hili ndio tatizo la Watanzania,kufanya kazi hawafanyi ila ni wa kwanza kudai malipo wakati wao ndio walikuwa wa kwanza kutofanya kazi kwa bidii na uadilifu,sasa wakatangazie vyumbani mwao.
 
Nimekuwa mfuasi wa kutoamini kufilisiwa kwa mali ya mdaiwa ila kuingia mkataba naye ila anaposhindwa au kukataa ndipo sheria ifanye kazi kutaifisha na kuuzwa kwa hizo mali.

Mkataba ninaousema ni kama assets zinahusiana na biashara yenye waajiliwa, hii ni biashara/kazi ambayo ukifilisi kuna wengine waliopo kazini nao watakosa ajira sababu ya mali kutaifishwa.

So jambo hili la mkataba linafanya walio kazini kuendelea na wale wanaodai kumiliki assets kwa kipindi cha deni huku wakishiriki katika baadhi ya maamuzi yanayoweza kuwata tija.

KUMBUKA: When you burn down old one, new thing grow up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…