ARUSHA: Kituo Cha Radio Five kufilisiwa, chadaiwa milioni 31.9... wafanyakazi waiomba mahakama kuuza Jengo na vifaa vya kurushia matangazo

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
622
1,000
Mahakama kuu masijala Ndogo ya kazi Kanda ya Arusha imeahirisha kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tan communication inayomilikiwa na waziri Mstaafu Edward Lowasa pamoja na kituo cha Radio Five na waliokuwa wafanyakazi Saba wa radio five wanaodai zaidi ya sh, milioni 31.9 baada ya kuachishwa kazi kinyume na utaratibu.

Wafanyakazi hao wakiongozwa na Geoffrey Steven walifungua kesi hiyo namba 151 ya mwaka 2020 baada kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama yausuluhishi (CMA) iliyompa ushindi mdaiwa.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Naibu Msajiri wa mahakama ,Ruth Masamu ilikuja katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa ,ambapo upande wa walalamikaji wakiongozwa na wakili Heri Makando walikuja kuiomba mahakama hiyo itoe idhini ya kukamatwa Mali za mdaiwa ambaye ni Tan Communication na kupigwa mnada ili kufidia malipo ya wafanyakazi hao.

Hata hivyo wakili wa upande wa mdaiwa,Andrew Maganga ameiambia mahakama hiyo kwamba amewasilisha notisi mahakama kuu ya rufaa kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Johannes Masara , June 16 ,2020 iliyowapa ushindi wadaiwa.

Naibu msajiri wa mahakama hiyo ,Ruth Masamu baada ya kupokea maombi hayo yaliyoambatana na notisi hiyo aliahirisha shauri hilo hadi Machi 16 mwaka huu.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Geoffrey Steven alisema kimsingi wamepokea kusudio la rufaa kwa upande wa wadaiwa na wanachosubiri no tarehe ya kusikiliza kwa rufaa hiyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa leo walikuja mahakani hapo kwa ajili ya kuiomba mahakama hiyo iweze kutoa idhini ya kukamatwa kwa Mali za mdaiwa ambazo ni Jengo la kituo Cha Radio five, lililopo Njiro ploti namba 153 na 154 block J , Jenereta,vifaa vya studio na vifaa vya kurushia matangazo.

Wadai wengine wa shauri hilo ni Monica Nangu , Gloria Kaaya ,Godluck Kisanga , Godfrey Thomas ,Akidai kilango na Josephzat Nyamkinda.


IMG-20210219-WA0105.jpg
 

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,953
2,000
Ni kweli tunadaiwa na hao wafanyakazi, ingawa si kiasi hicho cha fedha wanachosema. Hata hivyo tunaendelea na utaratibu wa kukata Rufaa. Kwa sasa nipo nje ya nchi, nikirudi nitashughulikia hili suala
Ha ha ha! Watu mnapenda sana kujipendekeza kwenye familia za wenye nazo, labda useme wewe Jane ni mtoto wa Kaka au mdogo wake na Lowassa na sio eti wewe ni mtoto wa Eddo! Nakataa tena kwa herufi kubwa! Watoto wa Edward Ngoyai Lowassa hawana hata mda wakushinda nakujibishana humu JF!

1. Fred Lowassa
2. Dr Adda Lowassa
3. Pamela Lowassa alishawahi fanya kazi BOT ni mke wa Sioi Sumari
4. Robert (Bob) Lowassa
5. Richard Lowassa!

Sasa kati ya Pamela na Dr Ada wewe ndiyo yupi sasa!
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,928
2,000
Ha ha ha! Watu mnapenda sana kujipendekeza kwenye familia za wenye nazo, labda useme wewe Jane ni mtoto wa Kaka au mdogo wake na Lowassa na sio eti wewe ni mtoto wa Eddo! Nakataa tena kwa herufi kubwa! Watoto wa Edward Ngoyai Lowassa hawana hata mda wakushinda nakujibishana humu JF!

1. Fred Lowassa
2. Dr Adda Lowassa
3. Pamela Lowassa alishawahi fanya kazi BOT ni mke wa Sioi Sumari
4. Robert (Bob) Lowassa
5. Richard Lowassa!

Sasa kati ya Pamela na Dr Ada wewe ndiyo yupi sasa!
Mkuu achana naye sisi TUMEMPUUZA !.
 

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,366
2,000
Hao wafanyakazi wnyewe hata kazi waliyokuwa wanaifanya hakua kama si kuuza sura na kufanya kazi za nje ya ofisi kwa kutumia ofisi kwa muda mrefu,na hili ndio tatizo la Watanzania,kufanya kazi hawafanyi ila ni wa kwanza kudai malipo wakati wao ndio walikuwa wa kwanza kutofanya kazi kwa bidii na uadilifu,sasa wakatangazie vyumbani mwao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom