Arumeru kwachafuka

Arumeru kwachafuka

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803









16 APRIL 2012

*Kauli za wagombea zachochea uvamizi wa shamba
*Wananchi waharibu mali, nyumba za wawekezaji
*Wadai kuambiwa mashamba hayo ni mali yao

Na Queen Lema, Meru

ZAIDI ya wakazi 300 waishio Kata za Maji ya Chai na Maroroni, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, juzi walivamia shamba la mwekezaji zaidi ya ekari 6,000 lijulikanlo kama Doll Estate.

Mbali ya uvamizi huo, wakazi hao waliwavua nguo zote walinzi wa shamba hilo, kuharibu mali na kuiba vifaa mbalimbali.

Akizungumza na Majira jana, Msimamizi wa Idara ya Wanyama katika shamba hilo, Bw. Robson Peter, alisema wakazi hao walifanya uvamizi huo saa 11 jioni.

Alisema wakazi hao walidai kuwa, shamba hilo ni mali yao kama walivyoambiwa na baadhi ya wagombea ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki.

"Wananchi waliovamia shamba hili ambalo linahusika na ufugaji wa wanyama mbalimbali kama twiga, swala, pundamilia na wengine walikuwa na silaha za jadi wakidai kuwa, hawataki kuona wawekezaji wa kizungu ndani ya shamba hili," alisema.

Bw. Peter alisema baada ya wananchi hao kuingia ndani ya shamba wakiwa wamevunja ukuta wenye urefu wa zaidi ya kilomita nne, waliwakamata walinzi, kuwavua nguo zote na kuwapa adhabu huku wengine wakiendelea kufanya uharifu wa mali katika nyumba za wawekezaji.

Alisema kutokana na uvamizi huo, walilazimika kutoa taarifa Kituo ch Polisi Meru ambacho kilituma askari ambao ndio waliofanya kazi ya kuwatawanya wavamizi hao kwa mabomu ya machozi.

Awali baadhi ya wawekezaji katika shamba hilo ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema kilichofanywa na wananchi waliofanya uvamizi huo hasa kutoka Kijiji cha Kitefu si cha uungwana kwani walikuwa wakiishi kwa ushirikiano mkubwa.

"Sisi tupo katika shamba hili kwa mujibu wa sheria, tunashangaa wakazi wa kata hizi kusema hawataki kutuona wakati sisi tuna haki, leo hii wamevunja nyumba zetu na kuchukua mali, hatujapendezwa na hali hii hata kidogo," walisema wawekezaji hao.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa kata hizo walisema kuwa, kuvamiwa kwa wawekezaji hao kunatokaa na kauli za siasa zilizotolewa na viongozi mbalimbali kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo.

"Juzi viongozi wa vyama viwili ambavyo vilikuwa vinachuana walidai haya mashamba ni mali ya wananchi ambao waliamua kwenda kufanya uvamizi ili kuchukua shamba hili, nguvu ya ziada inahitajika ili kukomesha tabia hii," walisema.

Diwani wa kata ya Maji ya Chai Bw. Loti Nnko, naye alijionea uharibifu wa mali za wawekezaji na kudai hadi sasa, thamani halisi ya uharibifu huo haijajulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye, amethibitisha kuwepo tukio hilo na kudai jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi zaidi.










 
Mikakati Ipangwe kuhusu hizo ahadi walizopewa wananchi; inaonyesha hayo mashamba au ardhi walinyang'nywa kwa nguvu na CCM; kulikuwa hakuna mawasiliano na wananchi wahusika.

Mmm Jamani tusifanye kama Kenya; Tuwe Watanzania tulinde Uhuru na haki za wananchi wetu
 
Walitakiwa wauwe muwezeshwaji mmoja......
 
Kwanini hawakwenda na Petrol wakaiteketeza kabisa hiyo kambi ya wawezeshaji wa nyonyaji?!!
 
sasa nimeamini watanzania wa leo sio wale wa mwaka 1961 wanambiwa kitu na kikifanyia kazi hivyo basi ni haki yao kudai mali zao
 
jama hilo eneo kikweli wamenyang'anya wananchi coz kulikua na barara inapita katikati ya hayo mashamba ya katani na ilitumika toka enzi sasa yale makaburu yameifunga barabara kitendo kinacho walazimisha wananchi kuzunguka umbali mrefu zaidi mfano kutoka kitefu kwenda usariva pia wametengeneza viwanja vya golf ragby na horse race ground vitu ambavyo haviwasaidii wananchi wa vile vijiji kwa sasa ni heri pangewekwa hospital coz tengeru ilipo hosptal ya rufaa ni mbali.naomba kuwasilisha.
 
jama hilo eneo kikweli wamenyang'anya wananchi coz kulikua na barabara inapita katikati ya hayo mashamba ya katani na ilitumika toka enzi sasa yale makaburu yameifunga barabara kitendo kinacho walazimisha wananchi kuzunguka umbali mrefu zaidi mfano kutoka kitefu kwenda usariva pia wametengeneza viwanja vya golf ragby na horse race ground vitu ambavyo haviwasaidii wananchi wa vile vijiji kwa sasa ni heri pangewekwa hospital coz tengeru ilipo hosptal ya rufaa ni mbali.naomba kuwasilisha.
 
wana Arumeru hiyo ardhi ni urithi toka wa wazee wenu so gawaneni ni mali yenu ILA kama ni la watanzania wenzenu acheni kama ni ya wazungu,wahindi, na waarabu yatwaeni haraka.
 
'Wawekezaji' wanafuga twiga, swala,.....nk! Kwa nini wasipelekwe tu kulekule Ngorongoro au Serengeti ndani kabisa ili wawafuge hukohuko??? $$§¿¤& zao.
 
Hivi ili la watu kufuga wanyama(zoo) karibu na Mbuga Momela(Arusha National Park) Mbona haingiii hakilini!

Mytake:Ukizungukwa na watu wenye njaa na shida na wewe ni tajiri kila siku unawanyanyasa kwa uwezo wako ipo siku watakubadilikia.Ndicho kinachowatokea hawa jamaa!Wananchi hawana Ardhi,wala Maji safi ya kunywa wao wanatumia Ardhi kwa kujenga kiwanja cha Golf kikubwa EAC and central Africa,Maji wao wanamwagilia ukoka wakati since Indepence wananchi wanaokaa jirani na eneo hilo hawajawahi kuona maji ya bomba...wanakunywa maji ya mto maji ya chai yemegeuza meno yako kama yamepakwa rangi!
 
sasa nimeamini watanzania wa leo sio wale wa mwaka 1961 wanambiwa kitu na kikifanyia kazi hivyo basi ni haki yao kudai mali zao

Ukisema watanzania unakosea maana huu mwamko siyo wa Tz nzima bali ni baadhi ya shm ktk hii Tz
 
Hi ndo Tz inayomjali mgeni kuliko mzawa na serikali yake inachukua maamuzi bila kuwashirikisha wananchi husika wa hilo eneo!
 
Duu kazi kweli kweli hii yote ni kazi CCM, wanachukuwa RUSHWA KUTOKA KWA HAWA WAWEKEZAJI UCHWARA na sasa imekuwa ni matatizo makubwaa..

Wanancho komboeni ardhi yenu
 
Back
Top Bottom