Ardhi Kliniki-Sumbawanga

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
264
Reaction score
151

Mkurugenzi Msaidizi wa Urasimishaji Makazi, Bw. Nicholaus Mwakasege, na Msajili Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa, Bw. Ng’umbunela Langalanga, wakitoa elimu kwa wananchi kupitia Vos FM ,90.1 FM Sumbawanga kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi, ikiwemo umuhimu wa kuwa na hati miliki, taratibu za umilikishaji wa ardhi, urasimishaji wa makazi, utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na matumizi ya Mfumo wa Kidijitali wa e-Ardhi.

Aidha, wataalamu hao wamewahimiza wananchi kutumia fursa za Kliniki ya Ardhi kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali za ardhi, huku wakisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata taratibu na sheria za ardhi ili kulinda umiliki wao na kuepuka migogoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…