SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,923
Bakwata mko wapi, wananchi wasio na hatia wanachinjwa na Assad lakini mmekaa kimya.
Jumuiya ya kiarabu ni vibaraka wa watu wa magharibi wapo kimya kumlinda Rais ambaye ni kibaraka wa marekani,hawana tofauti na BAKWATA Tanzania ambao ni vibaraka wakubwa wa serikali ya CCM wapo kwa ajiri ya kutukandamiza sisi muslim tangia enzi za uhuru,sasa ndiyo tumekuja kushtuka,waislam wenzangu safi na waliosoma elimu zote watakubaliana na mimi,wakumbuke hao viongozi,KULU NAFS DHAI KATUR MAUT
Dini ya jumlisha iko wapi au hakuna mafuta ndo maana hawasemi
Dini ya jumlisha iko wapi au hakuna mafuta ndo maana hawasemi
Hali ya Syria inasikitisha sana
Mkuu, Palestina tukumbuke hakuna mafuta
Rafiki zangu wa Syria nilionao hapa wanasema nchi yao inatengwa na Waarabu wengine kwa vile, Kiongozi wao yupo modern halafu ni wa dhehebu la Shia. Wanasema wana uhakika angekuwa Sunni, wangekuwa hata wameisaidia Syria dhidi ya Israel kwenye ugomvi wao juu ya Golan heights.
Anyway, labda ni hisia zao tu.
Ahamedinajad ni Shia, basi hata yeye amekuwa bubu wananchi hawa wanavyouawa? Ikumbukwe kuwa wanaouawa ni waislam kama waislam wengine kokote duniani na wanahitaji mtu wa kumkemea Al Assad ili aache kuendelea kuwachinja hawa raia wasiokuwa na hatia
Ndio. Ahamedinajad ni Shia. Lakini sio mwarabu. Kwa waarabu wenyewe, cha kwanza katika umoja wao kabisa ni uarabu (japo kibano kikizidi huwa wanaomba misaada kwa waislam wote). Hawa jamaa nilionao hapa wao wenyewe ni Sunni, na mtazamo wao ni kupata msaada na ushirikiano kutoka kwa waarabu. Ahamedinajad ni muislam, lakini si mwarabu, na kibaya zaidi yeye ni Shia.
Isitoshe kwa upande mwingine, Sehemu yoyote ambayo Ahamedinajad ata-support, automatically itageuka kuwa an enemy of the West. Na nadhani hata Assad analijua hilo. Iran ikiingia tu Syria, utasikia NATO wamepata kibali cha UN kulinda raia.
Mbele ya Mungu, ninaamini dini zote zinasema wanaofuta amri za Mungu wana haki sawa. Na kwenye international politics na UN human right declaration wanadai all men are created equal.Ahamedinajad ni Shia, basi hata yeye amekuwa bubu wananchi hawa wanavyouawa? Ikumbukwe kuwa wanaouawa ni waislam kama waislam wengine kokote duniani na wanahitaji mtu wa kumkemea Al Assad ili aache kuendelea kuwachinja hawa raia wasiokuwa na hatia
Mbele ya Mungu, ninaamini dini zote zinasema wanaofuta amri za Mungu wana haki sawa. Na kwenye international politics na UN human right declaration wanadai all men are created equal.
Kwa uzoefu wangu, hii ni tofauti sana "in practice".
utaona watu mpo dini moja lakini mnadharauliana. Hii ipo dini zote. Japo watu hawataki kukiri. Mbele ya Mungu mtu aliye Rwanda au Papua New guinea ana haki sawa na aliye ufaransa au Uingereza. Hiyo ni according to maandiko na imani. Lakini "in practice" utaona kunakuwa na "unequal treatment". Si ajabu kumwona mwarabu wa maana zaidi kuliko mndengereko hata kama wote mpo dini moja. Hii ipo TZ na ipo duniani kote.
Kwenye nchi kavu, Iran inapakana na moja tu ya kiarabu ambayo ni Iraq. Imetenganishwa kwa bahari na nchi kama Saudia, UAE, Qatar, Oman na Bahrain. Hizi zote ni nchi za Kiarabu. Majiran zake wengine ni Turkey, Turkmenistan, Afghanistan, Pakistan na Azerbaijan. Hizi pamoja na Iran wenyewe sio waarabu, ila ni largely Shia muslims.Nimekupata na ahsante sana kwa hizo facts kwani nilikuwa najua kuwa Iranians are arabs, kumbe they are not!
Kwa hiyo ni sababu zipi zilifanya watu waandamane hapa mjini kuhusu issue ya Libya?