Apple Yatangaza WWDC 2014

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159


​
Kampuni ya Apple yenye makao makuu yake huko Cupertino imetangaza mkutano wake mkuu wa waandika programu unaojulikana kama World Wide Developers Conference wa mwaka 2014. Mkutano huo utakaofanyika kwa muda wa siku tano utaanza siku ya Jumatatu, tarehe mbili ya mwezi Juni katika ukumbi wa Mostcone West.


Apple hutoa msaada kwa watengeneza programu za iOS na Mac OSX ili waweze kuimarisha kuborehsa, kufanya ubunifu na kutumia vyema teknolojia za kampuni hiyo. Apple itaweka wataalamu elfu moja kutoa msaada kwa watengeza Programu elfu tano watakaofanikiwa kununua tiketi za mkutano huo mwaka huu. Tiketi hizo zinapouzwa kupitia mtandao wa developers wa Apple humalizika chini ya muda saa moja. Uwiano wa developers watano kwa mtaalamu mmoja ni uwiano mzuri kwa mkutano mkubwa kama huu, hivyo watengeza programu wanatarajia kupata msaada wa hali ya juu kutoka kwa wataalamu wa Apple.


Mbali na kutoa msaada kwa watengeza programu, Apple pia hutumia mkutano huo kutangaza bidhaa mpya mbali mbali, baadhi ya bidhaa zlizotangazwa kwenye mkutano wa mwaka jana ni pamoja na Mac Pro mpya, iOS 7 na OSX toleo la Mavericks.


Watenenza programu wanaotaka kushiriki mkutano huo wanatakiwa kujisajili kabla ya tarehe nne mwezi huu. Wadau hao watatakiwa kulipia tiketi kwa jumla ya dola za kimarekani elfu moja mia tano na tisini na tisa. Apple inatarajiwa kuingiza karibu Dola za Kimarekani milioni nane kwa mauzo ya tiketi za mkutano huo.


Kwa mara ya kwanza Apple imetoa scholarship kwa wanafunzi wenye vipaji au uwezo wa kutengeza programu kushiriki katika mkutano huo, ambapo usajili wao utakuwa ni bure. Sharti la ushiriki ni kuwa na umri kati ya miaka kumi na tatu hadi kumi na saba, na pia watatakiwa kufuata masharti mengine ya scholarship hizo ambayo yameshatangazwa katika mtadao wa madevelopers. Hata hivyo wazazi wao watatakiwa kuwafanyia usajili wa kushiriki.


Wataalamu wa Apple watatoa mafunzo katika mkutano huo zaidi ya mia moja yanatakohusika na design, programu framework, graphics and games, location and motion, media, tools and performance pamoja na core OS za iOS na Mac OSX.


Apple pia watachagua washindi miongoni mwa watengeneza programu mbali mbali kwa mwaka huu, baadhi ya washindi wa mwaka jana ni pamoja na watengeneza programu za Sky Gamblers, Yahoo Weather, Procreate, Badland Evernote na Letterpress. Washindi hawa huchaguliwa kutokana na ubunifu, ugunduzi na matumizi mazuri ya teknolojia za Apple.


WWDC ni mkutano mkongwe katika fani ya gajeti kuliko mikutano yote na pia ni mkubwa kuliko yote. Google nao wanatarajiwa kufanya mkutano wa Google IO katika kipindi hicho hicho. Apple pia hutoa mualiko kwa wanahabari kushiriki katika mkutano huo. Hata hivyo swali kubwa kwa wateja ni bidhaa gani mpya itakayotolewa na Apple katika mkutano huo?
​

Chanzo: gajetek habari
 
Thanks Mkuu We miss You Mkuu Ulikuwa Wapi Kitamboo Millah
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kitambo sana tumekosa makala zako, karibu Tena.
 
Ahsanteni sana TZ boy na idawa majukumu tu, lakini tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…