Apple Wapata Haki-Miliki Muhimu kwa iPhone

Apple Wapata Haki-Miliki Muhimu kwa iPhone

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159


Mchoro wa haki miliki hiyo unaonyesha kwamba teknolojia ya kubinywa au kubanwa kwa simu iko kwenye gamba la simu yenyewe, teknolojia hiyo imeelezewa kama "Sensing capacitance changes of a housing of an electronic device". Pamoja na kuwa teknolojia hiyo imeonyeshwa kwenye simu, inaweza kutumika katika gajeti nyingine kama vile iPod, iPad na hata MacBook.

Mtumiaji ataweza kuipa amri mbali mbali simu kutokana na aina ya mbano (mbonyezo) na nguvu ya mbonyezo (pressure), Mfano uliotolewa katika matumizi ya aina hii ni kuibana simu yako pale inapoita iwapo unataka inyamaze bila ya kupokea simu au kama unataka uzime king'ora (alarm). Watumiaji watalazimika kujifunza aina ya mibinyo kwenye simu au gajeti nyingine wanazozitumia ambazo zitakuwa na teknolojia hiyo.


Teknolojia hiyo pia itahitaji msaada wa sensa nyingine ili kuweza kuifanya gajeti ielewe kama mbonyezo uliotokea umekusudiwa au ni wa bahati mbaya, yaani kwa mfano simu inapobanwa wakati iko mfukoni kutokana na kuikalia au mazingira kama hayo.

Apple iliomba haki miliki hii tangu mwaka 2011 na mwaka huu ndio imewaze kushinda umiliki wake, wakati kampuni mbali mbali zinapopata haki miliki huwa wanaziuza kwa kampuni nyingine, Apple huwa wanazitumia kwenye gajeti zao tu, isipokuwa pale sheria inapowalazimisha kwamba haki miliki husika ni shirikishi na hivyo wanalazimika kuiuza iwapo kuna kampuni nyingine inahitaji kuitumia.


Haki miliki katika gajeti aina ya simu na tablet imeleta vita vikubwa baina ya kampuni kama vile Samsung, Apple na HTC, imefikia hadi kampuni hizo kupandishana mahakamani mara kwa mara kutokana na madai mbali mbali. Kesi kama hizi zimeipelekea kampuni ya Google kuinunua kampuni ya Motorola, kampuni ambayo inaongoza kwa haki miliki nyingi zinazotumika kwenye simu za mkononi. Google ikitumia kampunia yake mpya ipo mbioni kutoa simu itakayojulikana kama X-Phone, ambayo inaaminiku kuwa ndio itakuwa simu kuu ya mwaka huu kwa upande wa Android (android flagship device)

Hata hivyo si kila teknolojia inayopewa haki miliki huwa inatumika kwenye gajeti, kuna teknolojia mbali mbali ambazo zimepatiwa haki miliki na kampuni kama vile Apple na hazitumiki, kampuni kubwa hufanya uwekezaji mkubwa kwenye utafiti na ugunduzi lakini tafiti nyingine huwa zinashindwa kupatiwa matumizi halisi katika gajeti, mfano mzuri ni kwa upande wa Samsung ambayo imeshapata haki miliki ya skrini zinazopinda, lakini kampuni hiyo bado inaendelea na utafiti jinsi ya kuitumia teknolojia hiyo.

Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia

 
Back
Top Bottom