ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
APR
20
[h=1]App ya Google Camera Kwenye PlayStore[/h]

Google inaendelea kuwapa chaguo wale ambao wananunua simu kama vile Samsung na HTC kutumia kutumia apps ambazo ni za asili za Android (Stock Android). Google camera imepokelewa vizuri na watumiaji wa Android kwani wengi waliopakua wametoa maoni mazuri kuhusu app hiyo ya kupigia picha. Kabla ya kuwekwa kwa app hiyo muda wa siku chache zilizopita, app hiyo ilikuwa inatumiwa na watumiaji wa Simu za Nexus na simu chache za ambazo hazikubadili kamera ya asili ya Android.
Kinachodhihirisha kuwa kamera hii imependwa na watumiaji ni kwamba mpaka sasa kuna zaidi ya watumiaji 15,000 ambao wameipa hadhi ya nyota tano katika kutoa maoni, huku walioipa nyota nne wanapindukia 6,500. Kwa wastani mpaka sasa app hiyo ina hadhi ya nyota 3.9 kiujumla. Hata hivyo pamoja na kupokelewa huko kuzuri bado ni mapema mno kwa kuwa na mtazamo halisi wa app hiyo, kwa vile app hiyo imetoka chini ya wiki moja nyuma.
Kinachovutia zaidi katika app hii ni uwezo wa ku-blur kile ambacho mpiga picha hujakikusudia katika picha na hivyo kuwacha kile ambacho kimekusudiwa katika picha kupata muonekano zaidi. Mbali na hilo mambo mengine yaliyo kwenye kamera hiyo ni ya kawaida kwa sasa kama vile panorama na photo sphere. Sifa kubwa nzuri ya app hii ya kamera ni jinsi ilivyo rahisi kuitumia ukilinganisha na zile za HTC, Samsung na simu pamoja na tableti nyinginezo za Android.
Hata hivyo watumiaji wa app hii hawataweza kutumia mambo maalum ambayo ni ya nyongeza kwa kamera za simu husiku, kwa mfano watumiaji wa Samsung Galaxy S5 au Samsung Galaxy Note 3 hawataweza kuchukua video za 4K, au kubadilisha focus ya taswira katika kamera ya HTC One M8 yenye lenzi mbili. Kwa wale ambao bado hawajapakua app hii wakongoli kwenye kiunga hichi app ya Google Camerakupakua app ya hiyo.
hata hivyo app hii inakubali simu ambazo zinatumia Andorid 4.4 toleo kitkat, hivyo iwapo bado unatumia Jelly Bean au Android za nyuma hutaweza kupakua App hii, tunaamini siku chache zijazo huenda ipapatika sehemu kama vile XDA Developers kwa watumiaji wengine, kwa sasa hawana budi kusubiri.

Chanzo: gajetek habari