Pongezi kwenu/kwako, hii ndio akili kubwa inayohitajika. kwa ushauri, isajilini Uganda, Burundi au Kenya; kufanikisha hilo, unaweza kutafuta mwanahisa mmoja kutoka kwenye hizo nchi.
Maoni yangu ni kuwa nimetazama mchoro wa app yenu hakika sijaona jambo jipya ambalo app inaweza tatua KATIKA ulimwengu huu ambalo hakuna mbadala wake Kwa asilimia 100.
Ubunifu wa technlojia Kwa Sasa ni lazima vijana mkaumize vichwa kuja na suluhu ya tatizo Fulani KATIKA jamii. Hayo yote KATIKA app yenu yana suluhu na apps nyingi zipo Kwa ajili hiyo.
Hata hao TCRA watafuata wenyewe tu iwapo app tayari ipo play store au Google play( ambako tcra siyo kwao) na sisi tunaichangamkia kutokana na kutatua tatizo Fulani.
Hizi issue za copy and paste idea bila kitu kipya au kwenda codeconyan kununua script za code na kuja kuunda sijui kama zinaweza tusaidia kama taifa.
Mfano. Kwa Sasa app inayokosekana bongo ni app ya kufanya escrow bussines. Mtu atakayeunda hiyo app atakuwa tajiri.
Kenya zipo.
Escrow ni mfumo kama mtu WA kati kati ya mnunuzi na muuzaji. Inaepusha wizi na utapeli ambao Kwa bongo ni mkubwa sana Kwa bidhara ya online.
Watu wengi wanauza vitu online lakini nani aanze kumlipa mwenzake ni kipengele. Ukimtumia pesa hatumi bidhaa au muuzaji akituma bidhaa kwanza mteja alipi. Hivyo mfumo WA escrow ungekuwa mkombozi sana.
Kama mnaweza unda escrow mkaingiza KATIKA app yenu itawainua hatari.