APP KWA AJILI YA VYUO VIKUU

dtj

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
1,332
1,375
Wazee salams! Mimi na wenzangu kutoka chuo kikuu cha DSM tume develop APP inayoitwa LAA.

App hii ipo mahususi kwa ajili ya wanachuo wote Tanzania na tayari iko inaoparate katika vyuo vikuu vitatu ambavyo ni UDSM, TUDARCO na MUHIMBILI huku bado tuna mazungumzo na vyuo vingene kujiunga na app hii.

KUHUSU LAA APPLICATION.

Sasa hakuna haja tena ya kutembelea mbao za matangazo chuoni, kwani LAA imerahisisha maisha ya chuo.

LAA itampa nafasi mwanafunzi wa chuo kikuu kupokea taarifa za chuo chake pindi zitakapo wekwa kwenye huu mtandao na wahusika.

Mara tangazo litakapo ingia kwenye simu ya mwanafunzi basi atapokea NOTIFICATION ya hilo Tangazo na pia atapata nafasi ya kucomment kuhusu tangazo hilo.


NAMNA INAVYOFANYAKAZI.

Application hii ina sehemu kuu nne
1) Annoncement
2)adverts
3)buy and sell
4) notes/ madesa

1.ANNOUNCEMENT
Hii sehemu ni kwa ajili ya matangazo ya kawaida kutoka uongozi wa chuo au serikali ya wanafunzi. Sehemu hii inaendeshwa na waziri husika wa mawasiliano katika chuo ambapo LAA ina oparate.

2. ADVERT
Haya ni matangazo makubwa ambayo hasa tumelenga kunufaika nayo kibiashara, kwa sasa sehemu hii inaendeshwa na ofisi za lodo group ambao ndio tumetengeneza APP hii.

3. BUY AND SELL
Hapa ni sehemu nzuri ya mawasiliano ya kibiashara kati ya wanafunzi wao kwa wao ambapo mwanafunzi ana uwezo wa ku upload tangazo lake na kuweka taarifa muhimu kuhusu bidhaa anayo uza pia anaweza kuweka picha hadi Nne kwa matangazo, sehemu hii kila mtu anaweza kuitumia iko free.

4. NOTES/MADESA
Hii sehemu ni kwa ajili ya kushare notes kama umepata desa basi unaweza kushare na darasa lako au kitivo chako na wanafunzi wenzako waka nufaika nayo.

NAMNA YA KUJISAJILI.

Kwa sasa LAA ipo katika play store lakini programmer yupo katika harakati za kutengeneza ya IOS

1) Download kupitia play store
2) Jisajili kwa kuandika
2a)Majina yako
2a1)Namba ya simu
2b) Namba yako ya usajili wa chuo(registration number)
2c) Jaza chuo chako
2d) jaza faculty au college yako.
3. Anza kupokea matangazo kutoka chuo chako.

APP hii ni rafiki kwa wanafunzi kwani haina ukubwa wa kujaza nafasi kwenye simu ya mtumiaji.


NAKARIBISHA MASWALI
 
Safi sanaaa, natumaini uongozi wa Wanafunzi na Vyuo watafurahi kurahisisha upelekaji wa taarifa. Big up
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Hizi ndio innovation zinazotakiwa kuletwa na wasomi wa level ya chuo kikuu. Hongereni kuanzia mweye idea mpaka developer wa hii App.
 
Mmetisha mno. Mpo serios nina ideal yangu long tyme kuhusu App. Sema sijapataga watu serious. Nitawataftaga by da way nice work
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Vizuri sana wakuu fanyeni mazungumzo na huku kwetu chuo cha st.joseph kilichopo hapa DSM kibamba tutashukuru sana kwa msaada wenu,,,,!!!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Back
Top Bottom