Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,609
Kuogelea mtoni ni hatari.Mto huwa na sehemu zile ambazo maji huwa yanazunguka Kama kiduara duara ulifika hapo unasimamishwa halafu unavutwa chini maji unaenda swekwa kwenye shimo ndani kabisa chini ambako huwezi ogelea hata ufanyaje. Utafia huko ndani maiti itaelea baadaye. Kuogelea mto watu huogelea sehemu chache Sana za mto.Uzembe sio? Nadhani hata kupigwa na radi ni uzembe wa kutembea kwenye mvua bila tahadhari au sio?
Hivi wewe Zinakutosha kweli?Sio uzembe sehemu hiyo ni hatari kuogelea hasa kwa wageniView attachment 1045233
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sehemu huwa na chunusi huwa zinaua Sana. Kuuliza Kwanza mihimu. Usipouliza ni uzembe ukajitosa tuUkitaka kuogelea kwnz kwenye mito waulize wenyeji kuna sehem nyengine sizakuogelea
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, jamaa kaniharibia kwaresma yangu, Shetani kabisa!Hivi wewe Zinakutosha kweli?
Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye Samwel James Chacha (25) amekufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Tukio hilo lilitokea Machi 7, mwaka huu na jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo
zilifanyika. Mwili wa marehemu ulipatikana Machi 11 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya imeeleza chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu.
Kuogelea mtoni ni hatari.Mto huwa na sehemu zile ambazo maji huwa yanazunguka Kama kiduara duara ulifika hapo unasimamishwa halafu unavutwa chini maji unaenda swekwa kwenye shimo ndani kabisa chini ambako huwezi ogelea hata ufanyaje. Utafia huko ndani maiti itaelea baadaye. Kuogelea mto watu huogelea sehemu chache Sana za mto.