Mleta mada na wanaJF wengine,
NHC wana utaratibu wa kuuza na kupangisha nyumba.
Hivyo kwa upande wa kuuza, mara zikiuzwa zinakuwa mali ya mmiliki na ni mmiliki tu ndiye ataamua nini afanye na apartment yake (aidha apangishe ama aishi yeye). Mfano wa hizi apartments ndio kama za pale Shekilango, Mchikichini, Upanga nk
Lakini kwa zile za kupangisha utaratibu uliopo ni kwenda kwenye ofisi ya mkoa ambao ungependa kupanga nyumba ( NHC uwa wanatambua Ilala, Temeke, Kinondoni na Upanga kama mikoa)....ukifika ulizia ofisi za estate....utalipia fomu ya maombi ya upangaji kiasi cha TZS 2500 na utatakiwa kujaza fomu hiyo ya maombi....kisha utasubiri mrejesho kutoka kwa maofisa wa NHC kukuarifu kama umepata upangaji ama lah.