Habari za Wakati huu;
Ni matumaini yangu mnaendelea salama na mapambano ya kiuchumi.
Je wewe ni mfanyabiashara wa kidigitali?Je wewe ni winga uliyepo kariakoo ambaye una connection ya wateja?
Leo nataka nikusanue Jambo.
Amua sasa kufanya Full ecommerce business.Badala ya kuwa mfanyabiashara ambaye unapost tu vitu labda kwenye magroup,status na kwenye mitandao kama instagram amua leo kuboresha biashara yako kwa kuanzisha duka kamili la mtandaoni.
Kwa nini ninakushauri hivi?Kwanza ni kwa sababu hivyo unavyofanya mtandaoni kwa kupost unasaidia kufanya Market Research na Market Development Sasa badala ya kusubiri mpaka ushindani ujae na matajiri wenye mitaje waingie kwanini usianzishe duka la mtandaoni?
Duka la Mtandaoni ni nini?
Duka la mtandaoni ni ukurasa maalum wa wavuti ambao unamuwezesha mnunuzi kuona bidhaa zako,kuagiza,kufanya malipo na kukamilisha mchakato wa manunuzi kwa njia ya mtandao.Baada ya kukamilisha muuzaji anaanza kushughulikia mchakato wa kuwasilisha mazigo wa mteja kwa kufuata maelekezo ya mteja.
Huhitaji duka la kuuza Tanzania nzima.Unaweza tu weka Duka la mtandaoni laa kuuza katika Mkoa wako tu.Lengo ni kupunguza mzigo wa majukumu na kadiri biashara yako inavyokuwa unaweza ongeza maeneo mengine.
Vile vile unaweza chagua kuamua kuuza bidhaa za aina tofauti kama mazao na nafaka pamoja mboga na matunda kwa kutegemea mahali ulipo.
Kumbuka hii kwa sasa huku kwetu ni fursa changa ila ndani ya miaka michache itakuwa FURSa kubwa na wenye mitajia wataivamia.Kwa sasa ukianza unapata fursa ya kujifunza na kukua zaidi.
Je Unahitaji kufahamu zaidi?Tutafutane kwa 0742405440