Anza au maliza siku yako kwa tafakari hizi muhimu siku ya leo

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
982
1,179
Maisha halisi na pekee kwa Mwanadamu ni yale ya kuwa Mcha Mungu, yaani kutii maagizo ya Mungu. Mambo mengine tuyaonayo hapa Duniani ni ubunifu tu wa Mwanadamu wa namna ya kuishi katika hii Dunia,ambayo kwa kiasi kikubwa hupelekea kumuasi Mungu.

Mabadiliko au Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ni njia rahisi zaidi ya kuingamiza Nafsi ya Mwanadamu ili isifikie ile hatma ya kweli iliyo kusudiwa.

Mafanikio au thamani ya maisha haipo katika misingi ya kufanikiwa kielimu, kufanikiwa kuwa na uelewa mkubwa wa Falsafa au Saikolojia kuhusu maisha ya Mwanadamu katika misingi ya ubinadamu au kufanikiwa kwa kuwa na kazi nzuri wala kufanikiwa kwa kuwa na utajiri mkubwa au kuwa mtu maarufu zaidi Ulimwenguni.

Iwapo thamani ya maisha ingetafsiriwa katika misingi ya mafanikio kupitia sababu tajwa hapo juu, basi walio jaliwa kuwa namna hiyo, wangeweza pia kutueleza kesho yetu itakuwa ya namna gani, au wangeweza hata kujiongezea siku za maisha yao au kuepuka kifo haswa kile kinachotokea kabla ya mtu kufikia hali ya uzee.

Mafanikio au thamani pekee ya mwanadamu yapo katika misingi ya kumjua Mungu, kufahamu maagizo yake, kuyashika na kuyatenda.

Si kila mwanadamu amejaaliwa kufahamu haya, ila Neema hii ni kwa walio wachache. Mwenye Masikio na Asikie.
 
Nimekimbilia nikajua bonge la thread nitakuta quotations za akina Aristotle, Eistein, Carl Max, Freud Sigmund, Adam Smith, Maria Montesori..... kwa tafakari zaidi. Kuchoshana tu,
 
Nimekimbilia nikajua bonge la thread nitakuta quotations za akina Aristotle, Eistein, Carl Max, Freud Sigmund, Adam Smith, Maria Montesori..... kwa tafakari zaidi. Kuchoshana tu,
Hapa hutokuta thread za namna hiyo. Thread kama hii ndiyo saizi ya Jukwaa hili. Hizo unazosema njoo kule "Jamii Intelligence" tutapeana quotations za kutosha. Kuna wenye kutumia quotations za hao uliowataja, vilevile na siye wazee wa Gombo tunatumia quotations za BIBLIA.
 
Mtoa mada una point kidogo, ila usikiogope sana kifo bali kiheshimu. Tambua uwepo wako hapa duniani na thamani yake. Kabla hujafa jiulize utakuwa umeongeza value gani kwenye hii dunia kwa manufaa ya kizazi kijacho? Elewa kuwa unafuu wa maisha tunaoufurahia sasa kama matibabu, usafiri n.k. unatokana na watu waliotangulia waliotambua hili.
 
Mtoa mada una point kidogo, ila usikiogope sana kifo bali kiheshimu. Tambua uwepo wako hapa duniani na thamani yake. Kabla hujafa jiulize utakuwa umeongeza value gani kwenye hii dunia kwa manufaa ya kizazi kijacho? Elewa kuwa unafuu wa maisha tunaoufurahia sasa kama matibabu, usafiri n.k. unatokana na watu waliotangulia waliotambua hili.
Hiki unachokiona ni maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, na kudhani inapelekea kurahisisha maisha hapa Duniani, ni muonekano wa jicho la kawaida sana. Lakini ukitazama mambo katika mwonekano wa jicho la tatu utagundua si kurahisisha maisha, bali ni kuyaharibu zaidi maisha. Hebu tazama mifano michache hapa chini..

1) Uharibifu wa Mazingira Duniani umesababishwa kwa kiasi kikubwa na Maendeleo ya Teknolojia hasa katika sekta ya Viwanda. Mabadiliko ya Tabia ya nchi na madhara yake kama vile mafuriko, baa la njaa, ongezeko la Joto, vimbunga, matetemeko ya ardhi kwa mujibu wa tafiti za kisayansi ya Kibinadamu ni mambo hatarishi yanayopelekea hatari kubwa ya maisha ya binadamu hapa Duniani. Wazungu wamefika mbali na kuona uwezekano wa kuishi kwenye sayari ya mars kwa kuhofia kuwa endapo Dunia itaharibika zaidi basi pawe na sehemu mbadala wa maisha.

Kwa muktadha huu, kwa jicho la tatu, faida za ugunduzi wa sayansi na Teknolojia hapa Duniani zina negativity kubwa zaidi kuliko faida zake. Maaana kama maendeleo ya sayansi na Teknolojia yanapelekea kuhatarisha maisha hapa Duniani ni hatari na hasara zaidi kuliko faida zake.

2)Hebu tazama visababishi vya cancer ambayo ni tishio kwa afya ya Binadamu. Kutokana na kinachosemekana ni maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kurahisha maisha kwa kuwa na chakula kilicho rahisi kubebeka na kulika, yaani vyakula vya viwandani, chakula pekee kinachangia asilimia karibia 70 ya visababishi vya cancer. Sasa Je, Jitihada za maendeleo uonavyo wewe zinatupeleka kwenye maisha hatarishi au maisha salama.?

3)Hebu tazama life span ya mwanadamu inavyozidi kupungua siku hadi siku. Haya yote yamesababishwa na ubunifu wa Mwanadamu kwenye hii Dunia.

4)Tazama hasara za mitandao ya Jamii ukilinganisha na faida zake. Wanaotumia mitandao kwa njia positive ni wachache zaidi kuliko wanao tumia kwa njia zilizo negative. Binadamu wamekuwa busy zaidi na maisha yasiyo halisi kwa kutekwa nyara kifikra kupitia mitandao hii. Watu wame concentrate usiku na mchana kuliko hata wanavyomtafuta Mungu. Kuliko wanavyotenga muda wao kufanya jitihada za kupata vipato n.k

Ubunifu wa Mwanadamu kwa kiasi kikubwa unapelekea uharibifu wa maisha ya mwanadamu kwenye hii Dunia kuliko faida.
 
Mtoa thread ungeweka na nukuu za Biblia ingesound vizuri zaidi
Kwanza tazama nukuu hii kutoka kwenye maandiko, " YESU akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate. Yule Kijana aliposikia neno lile,akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.(Mathayo 19:21-22)

Hakika tumepewa changamoto kubwa sisi Wanadamu hasa tunappodhani maisha ni kupambana ili tuwe matajiri. Anayedhani thamani ya maisha ipo katika Utajiri ni kupingana na kifungu tajwa hapo juu. Yesu anatupeleka kwenye maisha ya ujamaa zaidi(Socialism) kuliko yale ya mwenye nacho na asiye nacho. Jambo hili pia limesemwa katika Kitabu cha Matendo ya Mitume ...

Hebu soma kifungu hiki.....
"Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji, kwa sababu watu wote waliokuwa na viqwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. (MDO 4: 34-35).
Sasa ndugu ukisoma kwamakini vifungu hivyo, utapata wapi kiburi cha kudhani kuwa kuwa thamani ya maisha ipo kwenye utajiri na mali nyingi.? Vifungu hivyo vinaondoa kabisa dhana ya mwenye nacho na asiye nacho. Inaleta hali ya usawa kwa kila mwanadamu.

"Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote " (Mathayo 22:37).

Hakika kifungu hapo juu ni ujumbe mkubwa sana kwetu Wanadamu......Ukimpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, kwa roho yako yote, hakutakuwa na kitu kingine cha thamani katika maisha zaidi ya Mungu. Mungu atakuwa wapekee kwako na utampa kipaumbele kuliko hata mke wako, kuliko watoto, kuliko kazi, kuliko biashara na kuliko kingine chochote.

Umewahi kujiuliza, hivi kama Wanadamu tunampa kipaumbele zaidi Mungu, Je umewahi hata kutoa chozi mbele za Mungu kutokana na kumkosea Mungu.? Lakini ukifiwa na rafiki au ndugu utahuzunika sana na kutoa chozi hata kufikia kuugua kwa ajili ya nduguyo huyo. Ukipatwa na hasara ya mali au biashara utatoa hata machozi. Lakini ukitenda dhambi huwezi hata kujutia. Je, huko ndiko kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.?
 
Back
Top Bottom