Any Developing Country Can Do The following to Develop Faster

motonkafu

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2015
Posts
1,019
Reaction score
710
1. Linking rural areas and towns with tarmac road to enable the flow of raw materials from production areas to consumers.
2. Provide electricity power in all villages to where economic productive activities are largely done.
3. Build industries in production areas to enable fast processing of raw materials, also to cure the cost of transport.
4.Build schools and hospitals in villages so as to level the gap of availability social services in towns and villages.
 
Hiyo namba mbili ndio kila kitu. Unapoongelea link ya viwanda na na barabara, umeme wa uhakika ni muhimu sana kwenye kuendesha hivyo viwanda.
 
Hiyo namba mbili ndio kila kitu. Unapoongelea link ya viwanda na na barabara, umeme wa uhakika ni muhimu sana kwenye kuendesha hivyo viwanda.

Kabisa ndugu ndo maana kijijini wanashindwa kufanya uzalishaji wa tija kwa sababu ya kukosa umeme, kwa upande wa viwanda wale wenzangu tunaolima chai kule kusini watakua mashaidi viwanda viko town mbali na mashamba halafu Barbara ni mbovu kinachotokea wakati wa kusafirisha chai inaharibika sana
 
Hayo yote ni ya muhimu na yana nafasi zake kwenye jamii.

Huwezi kuwapa watu umeme wakati hawana elimu ya nini cha kuzalisha.
 
Hayo yote ni ya muhimu na yana nafasi zake kwenye jamii.

Huwezi kuwapa watu umeme wakati hawana elimu ya nini cha kuzalisha.
Safi sana, hapo hamna chochote cha kuacha nyuma, ili uchumi ukue kwa kasi kuna baadhi ya vitu vya msingi ambavyo hata vingine hajavitaja mleta mada.
Serikali yoyote ile inafaa kuhakikisha umeme wa uhakika, mawasiliano, maji safi ya bomba, elimu kwa watu wake, usafiri bora, usalama na amani n.k.
 
Kabisa wakuu bila kusahau sheria, katiba ia utawala bora
 
Rwanda wamefanya haya tayari wamefanikiwa
 
Kenya nao mkuu wako speed sana kutekeleza haya
 
sawa lakini umesahau elimu, maana kinacho tugharimu sana Tanzania na Africa ni ujinga uliopitiliza
 
Ipo no. 4 mkuu pamoja Huduma za afya
 
Hayo yote ni ya muhimu na yana nafasi zake kwenye jamii.

Huwezi kuwapa watu umeme wakati hawana elimu ya nini cha kuzalisha.
Nadhani kwa tulipo sasa, tuna wasomi wa kila namna hapa nchini, labda nawaha mazingira wezeshi ambayo yanaruhusu kuwekeza elimu yao kwenye uzalishaji halisi
 
Bila Kilimo hakuna maendeleo ni hatua kama mtoto anavyotambaa na kisha kutembea. Is the only economic activity ambayo kila mwanachi anaweza kupractice but we need market (local and international ) that is what Kenya is doing na sio nchi masikini tena..! Malaysia did the same.. Europe did the same.... KENYA are biggest export of Agricultural commodities kusini mwa jangwa la Sahara ukiondoa South Africa. Sis tunahimiza mbolea za ruzuku wanasiasa wapige... Kilimo cha mahindi na kula ugali ndio wanachokijua.. We have the land water, Rasilimali.. But they think with their balls.. Shame!!!!
 

True say mkuu ndo maana kuna Uzi niliwahi kusema somo la kilimo liafundishwe shuleni katikati levo zote, kwa huu Uzi hili wazo litajikita kwenye pointi ya kwanza niliposema 'to easen the flow of raw materials' mojawapo ya raw materials za kijijini ni mazao ya kilimo
 
Mkuu hapo umesema vizuri kabisa.. naamini magufuli atasoma.. au hata kijana wake akisoma asikose kumsimulia wakati wanapata chakula cha jioni
 
Nini maana halisi ya neno "maendeleo" katika nchi ya Kenya.?? Barabara za juu na ongezeko la deni kwa taifa.?? Kukithiri kwa vitendo vya rushwa na uvamizi dhidi ya raia wa kawaida.?? Aina gani ya speed inatumika kutekeleza haya.!!

Wamejitahidi sana kusambaza umeme vijijini , pia wakulima wa chai wa Kenya wametupiga bao parefu kuna bwana shamba aliniambia wakulima wa chai Kenya wanafwata weather statistics kujua kama chai inatakiwa kuchuma wakati bongo kila mkulima anaenda shambani kuchungulia kama tayari au bado
 
Asante mkuu kwa uchambuzi yakinifu.kwa hiyo rwanda tuiweke katika kundi lipi developing countries or developed countries
 

Mkuu umesahau Kenya July wametoka kwenye ulimwengu wa tatu sasa wapo kwenye kundi la nchi zenye uchumi wa kati kwa nini isiwe tz, tumetaja izi nchi mbili kama mfaano wa kuiga kwa ukanda huu tuige mazuri mabaya tuache mf. Tunaweza tukaiga Kenya kwa kurudisha somo la kilimo shuleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…