ANGUKO CCM S/MITAA: Mabalozi wa nyumba kumi '10' wana thamani gani sasa?

Japo sio mwanachama wa chama chochote, lakin mabalozi wa nyumba kumi wanasaidia sana usalama, hasa wahamiaji haramu,
 
Ukweli ndio huu UKAWA wamechukua mitaa yote huku kwetu. Je, shughuli za mjumbe wa nyumba 10 CCM zitaendelea kutambulika?


KATIBUA Usiulize kama haujui USALAMA wa MWANANCHI unaanzia wapi... Angalia KENYA wanavyojutia na kutamani MFUMO wetu wa kisiasa wa BALOZI NYUMBA 10 zinazofahamu wageni wa Maeneo yetu wanaishi wapi hivyo rahisi kutambua UGAIDI au UJANGILI au UUZA MADAWA ya kulevya...

Nadhani hata UKAWA hawata ONDOA hiyo...

Marekani wao wanampa kila mtu number... ukihama na kuhamia sehemu nyingine hiyo number yako inakufuata... kama uligonga mtu record ipo - kama uliiba ipo kwenye hiyo number
 
Ninachouliza sio kufutwa huu utaratibu! Ila utaratibu wa wajumbe wa nyumba kumi kutoka upinzani nao utaanza au walewale?
 
huku Arusha sisi tumeamua mabalozi wote wanafutwa na watu watachukua fom na kugombea upya wa vyama vyote, na atakaeshinda anakuwa balozi wa serikali sio wa chama tena
 
Kuna mtaa wa kizaboni songea kuna wajumbe wa nyumba kumi wa ccm na pia chadema. Na mambo yanaenda vizuri tu kwa kuwasaidia wanachama wao kwenye masuuala ya kijamii. Nionavyo mm ni mfumo mzuri sana kiutawala kama nngu alivyosema. Hata kichama husaidia sana kimkakati wa ushindi kwani hujua kati wa wananchi wake wangapi ni wapiga kura. Nakumbuka nilikosa sale za ccm kwa kutoshiriki vikao hv. Nashauri huu mfumo uendelezwe tu.
 
Ninachouliza sio kufutwa huu utaratibu! Ila utaratibu wa wajumbe wa nyumba kumi kutoka upinzani nao utaanza au walewale?

Balozi nyumba kumi ni nafasi ya kiuongozi ya chama cha mapinduzi haitambuliki kiserekali ingawa kwa uelewa mdogo wa wananchi huyu balozi alitumiwa sana na viongozi wa serekali za mitaa kumthibitisha mtu kabla hajapatiwa huduma katika ofisi za kijiji .Kimsingi CDM wasiendelee kuwatumia hawa kwa maana ni makada sana ni vizuri kuwaacha waninginie bila majukumu ili kuifuta ccm na kuzipa nguvu ofisi za mitaa na kijiji.
 
Ukweli ndio huu UKAWA wamechukua mitaa yote huku kwetu. Je, shughuli za mjumbe wa nyumba 10 CCM zitaendelea kutambulika?

Mabalozi wa nyumba kumi kumi tangu awali hawakutakiwa kuwa viongozi wa chama. Ni viongozi wa serikali ila unfortunately CCM wamewatumia kama viongozi wa chama kwa manufaa yao. Discussion ya kama wanahitajika au la ni jambo la kupeleka bungeni kwa sababu ndilo lenye mamlaka ya kujadili mfumo wa serikali zetu. Mimi ningefikiri ofisi za kufumua kwanza ni zile za RC na DC kwa sababu tunao wakurugenzi ambao ni watekelezaji kwenye level hizo.
 
Back
Top Bottom