Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Watu 17 wameripotiwa kufariki na wengine 60 kujeruhiwa vibaya baada ya mkanyagano kwenye uwanja mmoja wa mpira nchini Angola.
Mkasa huo umetokea katika mji wa kazkazini mwa nchi hiyo Uige na taarifa hizo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiandamana na picha.
Mechi iliochezwa ilikuwa baina ya timu za Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo,
Inadaiwa kitendo cha kundi la mamia ya watu la kuingia kwa nguvu kwenye uwanja huo ndio kilichosababisha mkasa huo.
Msemaji wa hospitali ambako waliojeruhiwa wanatibiwa amesema vifo vya wengi vilisababishwa na kukanyagwa huku wakikosa hewa ya kupumia.
Tayari rais wa taifa hilo Jose Eduardo do Santos ameamrisha uchunguzi kufanywa.
Daktari mmoja amesema kuwa watu kadhaa walikosa hewa huku wengine wakiwakanyaga wengine ili kujinusuru.
Mechi hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya msimu katika ligi ya soka nchini humo.
Chanzo: BBC/Swahili