Angekuwa wewe ungefanyaje?

Wema usizid uwezo mkuu utakuja ufe maskini eti ukiamini Mungu atakubarik,utabak kuwa tajiri wa imani huiu unalala njaa
 
Kama hizo hela huwezi kuzipata tena hata baada ya miaka mitano usimpe, fanya biashara, huwezi kumaliza changamoto zote humu duniani, fanya sehemu yako ila usivuke mipaka, jifunze kusema hapana na ubaki na mtizamo chanya.
 
Hizo pesa ungewapa hao dada zako waliyoolewa maana wanavuja jasho huko...
 
Ukitaka kupata pesa lazima utoe watu kafara,sasa ili ufanikiwe unatakiwa usitoe msaada wowote kwa huyo mzee akifa wewe ndo utafanikiwa

NIAMINI MIMI
 
Mwambie rafiki yako nae aumize kichwa jinsi ya kupata pesa. Anataka utelezi bila ya yeye kuumiza kichwa. Kama mtu wa karibu weka mchango wako ila rafiki yako pia kama wafamilia wafanye jambo.
 
Kama inawezekana washirikishe wazazi waliokupa hizo pesa juu ya hilo, kama wataona sawa kusaidia basi haitakuletea shida, ila ukijiamulia mwenyewe mkuu naona jinsi utakavyokosana na ndugu zako pengine na huyo rafiki pia. Poleni
 
hela sio zako washirikishe kwanza waliokupa hizo pesa, ingekua ni zako wewe binafsi umezitolea jasho sawa, lakini hizo ni hela za wazazi wako washirikishe kwanza na umwambie rafik yako.
alafu kwani huyo rafik hana Ndugu kabisa wakupitisha mchango kuongezea ongezea au
 
Usimpe zote , mpe zile ambazo kwa nafsi yako uliona utaweza kumsaidia nyingne aombe kwa ndugu wengne.
 
Ndugu zake wakae kikao wajue namna ya kumsaidia huyo mgonjwa, rafiki yako ni mbinafsi, kwanza kabisa umemkaribisha kwenye mpango wa utafutaji sahivi anakushawishi mtumie mtaji kwa ajili ya baba ake kwani hana ndugu wengine?! Mpe mchango kidogo asiposhukuru mkimbie mana kuna watu wengine wapo kwenye maisha ya wenzao kwa ajili ya kuwatumia tu, yeye angeweza?
 
Huo ni utumwa wa fikra, pesa za biashara zibaki kwenye biashara hilo wala usipepese macho kabisa.
 
Ndugu kwisha jua umekwisha

Mwambie mwanao kuwa hizo pesa ni za familia co zako
 
Sometimes maisha yanahitaji kuwa na roho mbaya kiasi. Kila nafsi itaonja umauti na kumtibu Mzee haimaanishi akipona atarudisha, Kama wakufa na afe tu ila toa kile ambacho nafsi Yako itaridhia. Kama ni robo, theruthi au nusu toa na mengine watahangaika wenyewe.

Sometimes mnaweza mkarisk mtaji wote na mtu akatembea mkakosa hata hela ya jeneza. Vipi kuhusu familia Yako ambayo wamekuamini na wanaamini ukiimarika kiuchumi utawasaidia Leo umeuguzia mtu pesa yote! Yaani mkaja wa mama ambae amelea kuanzia mimba mpaka Binti ameolewa wewe Leo uchezee! Basi Bora uirudishe Kama imekushinda kuiendeleza.

Rafiki atakushukuru Kama ukimpa hela yote na baba yake akipona itakua vema zaidi na akifa ndo basi Tena. Lakini siku moja atakuja kupewa umbea kuwa unatembea na mkewe au kisa chochote, mtagombana Kama hujawahi msaidia. Wema uwe na kiasi ndugu yangu.
 
Kumpa yote ata yeye asingeweza, mpe wazo la kupitisha mchango kwenye familia yako na yake na kwenye nyumba zenu za ibada, urafiki ua hauna guarantee
 
Haya maisha rafiki wa Kweli ni wazazi wako tu Jifunzee kuwa n maamuzi magumu usitoe hata mia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…