Angalizo Kwa wanamaombi Kwa Katiba

Angalizo Kwa wanamaombi Kwa Katiba

Wa Mjengoni

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2010
Posts
480
Reaction score
128
Viongozi wa dini na walokole wenzangu Bwana Yesu Asifiwe!

Naomba kabla hatujaombea Katiba iliyopendekezwa ipite kujaribu kwanza kuangalia vipengele vilivyoko humo kama vina reflect kumtumikia shetani au laa. Mfano jana Jaji Warioba amesema upande wa tunu na maadili ya viongozi Katiba pendekezwa haiwazuii kujirundikia mapesa haramu nje ya nchi, yaani ruksa.

Sasa Mlokole unapoombea kwa dhati kabisa mpaka unalia jambo hili una maana gani kama sio sawa na kumuombea jambazi anayetaka kwenda kuvunja duka afanikiwe? Najua wengi wanaomba bila kufahamu sawasawa wanayoyaombea ndani ya hiyo pendekezwa.

Nimesema hili kwa sababu leo asubuhi nimeona Ch. 10 taarifa ya habari maombezi ya Kanisa la Moraviani Katavi.
Ni bora maombi yakaishia katika kusema "Mungu tuongoze ktk kupata Katiba bora" finish...bila kuongeza neno "iliyopendekezwa."

Mungu awabariki na awape hekima.
 
Yaani kuna saa huwa hawa viongozi wa dini tena wooote wameyaacha maandiko na kuusimamia unafiki mfano wanajua kabisa katiba ccm ndio wameacha maoni ya wananchi na kuweka ya watawala halafu wanazunguka mbuyu kwa kuomba amani kwa nini wasiwakemee hawa wanasiasa wanajulikana kabisa ndio wanaofanya mpaka tufike hapa.
 
Kwa hatua hii tuliyofikia unapoomba sidhani kama unakuwa unaombea upatikanaji tena maana kupatikana tayari imeshapatikana.....mi nadhani kilichobaki ni kuombea mapenzi ya Mungu yatimizwe kama itampendeza ipite hiyo na ipite kama haimpendezi haitopita. Cha zaidi sana ni kuomba amani itawale kwenye michakato yote maan pua zangu zimeanza kunusa harufu ya damu mpaka sasa
 
Mtoa post umezungumza kitu cha ukweli maana kuna viongozi wengine wadini hawajielewi kabisa wanatumika tu hovyo,, bila kuchanganua mambo,,, "watanzania wanahitaji mabadiliko" by the late mwl nyerere
 
Mtoa post umezungumza kitu cha ukweli maana kuna viongozi wengine wadini hawajielewi kabisa wanatumika tu hovyo,, bila kuchanganua mambo,,, "watanzania wanahitaji mabadiliko" by the late mwl nyerere

Kuna wakati kwa kila jambo... Wakati wa kulia,kucheka nk. Maombi yafuate mapenzi ya Mungu na mahitaji ya jamii.
Sasa mtu kuombea amani,ili hali unajua wizi mkubwa wa mapesa unafanywa na watawala,njama nzito zinapangwa na wachache kuwakandamiza wanyonge nk. si sahihi.Maombezi yalenge mahitaji ya jamii na mapenzi ya Mungu. Mfano; zaburi 123 ni mwelekeo wa mahitaji ya kila mtanzania mwenye haki:
" 1.Nimekuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
2.Kama vile macho ya watumishi kwa mkono wa bwana zao. Kama macho ya mjakazi kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
3. Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.
4. Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha,Na dharau ya wenye kiburi."
Wakati huu roho ya machafuko inatamalaki duniani kwa sura tofauti za dharau,kiburi na mzaha kupitia siasa, uchumi,dini na mambo ya kijamii. Hivyo tuungane kuomba nguvu za Mungu ziharibu.mipango ya roho iliyozagaa kote.
 
Viongozi wa dini na walokole wenzangu Bwana Yesu Asifiwe!

Naomba kabla hatujaombea Katiba iliyopendekezwa ipite kujaribu kwanza kuangalia vipengele vilivyoko humo kama vina reflect kumtumikia shetani au laa. Mfano jana Jaji Warioba amesema upande wa tunu na maadili ya viongozi Katiba pendekezwa haiwazuii kujirundikia mapesa haramu nje ya nchi, yaani ruksa.

Sasa Mlokole unapoombea kwa dhati kabisa mpaka unalia jambo hili una maana gani kama sio sawa na kumuombea jambazi anayetaka kwenda kuvunja duka afanikiwe? Najua wengi wanaomba bila kufahamu sawasawa wanayoyaombea ndani ya hiyo pendekezwa.

Nimesema hili kwa sababu leo asubuhi nimeona Ch. 10 taarifa ya habari maombezi ya Kanisa la Moraviani Katavi.
Ni bora maombi yakaishia katika kusema "Mungu tuongoze ktk kupata Katiba bora" finish...bila kuongeza neno "iliyopendekezwa."

Mungu awabariki na awape hekima.

Hopeless, Syria, Iran, Iraq, etc hakuna sala mbona kuna vita kila leo. What is sala? Shetani ansikia sala? Ni mapambano ndio utapata haki yako na si sala.
 
Hopeless, Syria, Iran, Iraq, etc hakuna sala mbona kuna vita kila leo. What is sala? Shetani ansikia sala? Ni mapambano ndio utapata haki yako na si sala.

Upo nje kidogo ya mada yetu: Ni hivi sala isikike kwa Mungu au isipokelewe hapa sio mjadala wetu.

Mjadala ni je wale wanaofanya sala za kuombea kupita kwa Katiba iliyopendekezwa wana uelewa na wanachokiombea?
 
Uko sahihi mkuu.mara nyingi walokole tunajitoa ufahamu kabisaa...hata kufikia hatua ya kufanya maombi yasiyo na mwelekeo au ya kinafiki.Mungu atusaidie sana
 
Upo nje kidogo ya mada yetu: Ni hivi sala isikike kwa Mungu au isipokelewe hapa sio mjadala wetu.

Mjadala ni je wale wanaofanya sala za kuombea kupita kwa Katiba iliyopendekezwa wana uelewa na wanachokiombea?

Whatever the case, ninakuelewa ulicho maanisha. On top of that -kuombea kupata katiba bora, nasema sala hazisaidii kumbadilisha shetani, ni kupambana naye physically, na sio kwa sala. Katiba bora haitapatikana kwa sala!
 
Back
Top Bottom